Sunday, December 29

HABARI PICHA: KUNDI la Pili la watalii wafika Kisiwani Pemba.

MKUU wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja na Afisa Mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba Zuhura Mgeni, wakiwapokea baadhi ya watalii 107 waliowasili Kisiwani hapa 88 kati yao ni kutoka Marekani
MMOJA ya watalii waliowasili katika bandari ya Mkoani kwa kutumia Meli maalumu, akipokea shambi kutoka kwa mmoja ya wasanii kutoka kikundi cha Ngoma ya asili ya Mkota ngoma ya Wilaya ya Mkoani
WASANII wa Kikundi cha Ngoma ya Asili Mkota Ngoma kutoka Mkoani, wakitoa burudani ya ngoma hiyo, kwa watalii 107 waliowasili Kisiwani Pemba 88 ni kutoka Marekani
BAADHI ya watalii waliowasili Kisiwani Pemba 107 huku 88 kutoka Marekani, wakiangalia ngalia ngoma ya asili ya Mkota Ngoma kutoka Mkoani ikitoa burudani wakati walipowasili katika bandari ya Mkoani
AFISA Mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba Zuhura Mgeni, akizungumza na baadhi ya watalii waliowasili katika bandari ya Mkoani kwa lengo la kutembelea ndani ya Kisiwa hicho

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)