Saturday, January 4

Wasaidizi wa sheria kuwezeshwa kufanya kazi zao kwa uweledi na ufanisi mkubwa.

NA ABDI SULEIMAN.

WIZARA ya Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utwala Bora, kupitia idara ya katiba na msaada wa kishria Zanzibar, imesema imeandaa mpango imara wa kuwawezesha wasaisizi wa sheria kuweza kufanya kazi zao kwa uweledi na ufanisi mkubwa.

Hayo yameelezwa na Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Pemba, Halima Khamis Ali wakati alipokua akifungua kiko kazi cha kujadili rasimu ya mpango huo, kilicho washirkisha wadau kutoka sekta mbali mbali za sheria kisiwani Pemba na kufanyika mjini Chake Chake.

 

Alisema Wizara kupitia kidara ya katiba, imeona ipo haja ya kuweka mpango mkakati wa miaka mitatu, ili kuandaa mazingira mazuri kufikia malengo na kuleta mageuzi, huku mpango huo ukiwa na malengo 10 ya  kufikia pale panapohitajika.

 

“kikao hichi ni cha kupokea maoni yetu sisi wadau, mpango mkakati unahitaji kuchangiwa ili kuboreshwa zaidi, ili uweze kuleta tija ya haraka, mikakati itakua na manufaa kwa taifa,”alisema.

 

Aidha Mdhamini Halima alisema serikali imeona juhudi za watoa msaada wakisheria na kuondosha vikazo dhidi yao, wakati idara ya katiba na msaada wakisheria ikiendelea kufanya vizuri katika majukumu yao ya kazi.

 

Hata hivyo alimpongeza mkurugenzi wa idara ya katiba na msaada wakisheria Zanzibar, kutokana na kuisimamia vyema idara hiyo pamoja na kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.

mapema akiwasilisha mpango huo kwa wadau mbali mbali, afisa  sharia kutoka idara ya katiba na msaada wa kishria Zanzibar Ali Haji Hassan, alisema lengo la mpango huo ni kuwepo kwa mazingira rafiki ya upatikanaji wa huduma za kishiria hususana kwa watu wenye mahitajimaalum.

 

Alisema kwa sasa wapo watoa msaada wakisheria wanaofundisha kwa kutumia lugha za alama, ambao huambatana katika maeneo mbali mbali ili wasaidia wananchi viziwi.

 

“Haya ni mafanikio makubwa kwa idara ya katiba na msaada wakisheria Zanzibar, kuwa na watoa msaadawakisherai wanaotumia lugha za alama,”alisema.

 

Alisema kupitia mpango huo wasaisizi wa sheria watakua na mazingira bora na rafiki ya kufanyia kazi na kuketa tija kwa taifa.

 

Hata hivyo aliwataka wadau wa mpango huo, kuhakikisha wanatumia fursa yao ya kutoa maoni ipasavyo ili mpango huo uweze kwendana na mabadiliko yaliyoipo katika utoaji wahuduma.

wakitoa maoni yao wadau hao wameishauri idara ya katiba na msaadawakisheria Zanzibar, kuwangalia kwa karibu zaid watu wanao toa msaada kishria kuwepo na sheria itakayowalinda wakati wa kutekeza majukumu yao.

 

Rashid Hamad kutoka Chuo cha Mafunzo Pemba, aliitaka Idara ya Katiba na Msaada wakisheria Zanzibar, kujitolea kutoa ufadhili kwa wasaidizi wa sheria kusoma digiri ya sheria ili waweze kuwasaidia wananchi wanaohitaji huduma za kisheria bure.

 

“Sisi kule kwetu kuna vijana wale walioko rumande kuna siku walitaka wakili, nilipompigia wakili alinambia akija huko mpaka nimpatie pesa, sasa idara bora musomeshe tu  maana kwa kutegemea mawakili hawa watu watakosa haki zao za kisheria,”alisema.

 

MWISHO