NA ABDI SULEIMAN.
MWENYEKITI wa UWT Taifa Mary Pius Chatanda, amesema wanakusudia kuanzisha dawati la wasaidizi wa sheria katika ofisi za UWT, ili kuwasaidia wanawake na watoto wanaokumbana na changamoto za udhalilishaji na kuhitahi huduma za kisheria.
Alisema dawati hilo litaanzishwa katika ofisi za UWT Tanzania nzima, ili kuwasaidia wanawake wanaokumbana na matatizo hayo kwa kuogopa kwenda mahakamani au kutokuwa na uwezo wakupata wakili.
Aliyaeleza hayo hivi karibuni Kisiwani Pemba, katika mkutano wa hadhara wa siku wa mwanamke Duniani uliohudhuriwa na wanawake kutoka sehemu mbali mbali.
“Nawaagiza nchi nzima kuanzisha jambo hili, kuhakikisha wanawatafutwa mabinti ambao wamesoma mambo ya kisheria na hawana kazi zozote na wapo majumbani, hawa tunataka kuwaunganisha na Ofisi za UWT na kuwakabidhi majukumu,”alisema.
Alifahamisha kwamba majukumu ya wanasheria hao, ni kuwasikiliza wanawake wenzao wenyechangamoto za kisheria, ili kuweza kupatiw aufumbuzi wachangamoto zao.
“Viongozi muliochaguliwa tuone namna gani ya kuwapata vijana ambao wamesomea masuala ya kisheria, kwa wiki wanaweza kusikiliza mara moja na wanawake wengi, wataona wametendewa haki kwa kiasi kikubwa, tunaposema tuwe karibu na wanawake ni pamoja na jambo hili, la kuwasaidia katika masuala ya kisheria,”alifahamisha.
Mwenyekiti huyo alisema kwa kuazia wanaweza kuanza na wananchi 20 hadi 30 kuwapatia msaada wa kisheria, baada ya kuwasikiliza changamoto zao, kama kupelekwa mahakamani wato watakua ndio wanasheria wao wakuwasimamia.
Alisema wapo wanawake wanaokwenda mahakamani wanashindwa kesi zao au wanaogopa kwenda mahakamani, lakini wakiona kuna dawati la kisheria katika ofisi za UWT tumewaweka wanasheria wako pale na wanasikiliza changamoto zao, basi wanawake wengi wanaweza kuwa kimbilio ni UWT.
Aidha alisema jambo hilo likifanyika itakuwa wamewasaidia wanawake wengi sana tena kwa wakati mmoja, wataweza kuwahimiza wanawake wenzao na kuja kupatia ufumbuzi wakisheria.
Kwa upande wao baadhi ya wanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto Pemba, wamepongeza uwamuzi huo waUWT kuanzisha dawati la msaada wakisheria kwani litaweza kuwasaidia wanawake wengi.
Dina Juma kutoka PEGAO amesema huo ni uwamuzi sahihi wa kuwa na dawati hilo, kwani wanawake wengi wamekuwa wakikamwa kwenda kupata haki zao mahakamani kutokana na sababu mbali mbali.
Alisema wapo baadhi ya wanawake wanaona tabua kueleza uhalisia wa mambo yao, kutokana na waendesha mashtaka au wanasheria kuwa ni wanaume.
“Kama kutakua na wanawake watu basi wanawake wengi watakua wawazi kueleza uhalisia wa madhila ya udhalilishaji wanaofanyia,”alisema.
Naye mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wakisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema idara ya katiba na msaada wakisheria inaendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma ya msaada wa kisheria ili kuweza kutekeleza majukumu yao vizuri na kuwasaidia wananchi wanyonge wenye mahitaji ya kisheria.
MWISHO