Mhe. Hemed ameyasema hayo alipofanya ziara ya kukagua shughuli za ushushaji wa Makontena Bandari ya Malindi pamoja na kukagua maeneo yanayowekwa makontena katika Bandari kavu ya Bwawani na Maruhubi Jijini Zanzibar.
Amesema ni hatua ya kufurahisha kuona Shirika hilo limetenga maeneo ya kuweka Makontena kwa mujibu wa mchanganuo wake ili kupunguza mrundikano Bandarini.
Amesema ni vyema kwa Taasisi husika kuweza kushirikiana pamoja ili kurahisisha huduma kwa wafanayabiashara kutokaa muda mrefu bandarini kwa mujibu wa Sheria.
Aidha amewataka watendaji wa Shirika la Bandari kufanya kazi masaa Ishirini na Nne (24) ili kupunguza siku za kukaa meli Bandarini.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameutaka Uongozi wa Shirika hilo kuhakikisha kila Mfanyabiashara anaedaiwa kwa kuchelewa kutoa Makontena analipa kwa mujibu wa sharia.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema uharakishwaji wa utoaji wa Makontena Bandarini utasaidia kuiongezea Serikali mapato na kuweza kuwashawishi wafanyabiashara wengine kuongeza idadi ya Meli na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa nchini.
Katika Ziara hiyo Mhe. Hemed ameuagiza Uongozi wa Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi kulitoa Kontena moja lenye Mchele Mbovu kati ya Makontena matano lililobaki Bandarini na kuchukua hatua stahiki kisheria ikiwa kuurejesha ama kuuangamiza.
Nae Waziri wa ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Dkt. Khalid Salum Muhamed ameeleza kuwa Wizara kupitia Shirika la Bandari limetatua changamoto zilizokuwa kikwazo bandarini hapo ikiwemo Vifaa vya kushushia kontena, eneo la kuweka makontena yenye mizigo, pamoja na eneo la kuweka makontena matupu.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndugu Nahat Muhamed Mahfoudh ameeleza kuwa Shirika tayari limenunua mashine za kushushia Makontena ili kuongeza ufanisi wa kazi.