Friday, January 10

ZEMA yateketeza tani 1.5 ya vifuko vya plastiki Pemba vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 10

MAMLAKA ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA)Ofisi ya Pemba, leo 22/3/2023 imeteketeza vifuko vya plastiki tani 1.5 vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 10, mali ya mfanya biashara Mohamed Juma Ali mkaazi wa Kiuyu Minungwini.

Vifuko hivyo vimeteketezwa katika  eneo la kwareni Vitongoji Wilaya ya chake Chake, baada ya mahakama Wilaya ya Wete kumtia hatiani na kuamuru kuteketezwa.

Zoezi hilo la uteketezaji limeweza kushuhudiwa na viongozi mbali mbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.