Friday, November 15

JET yawataka watanzania kuendelea kulinda misitu

MKURUGENZI Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) John Chikomo akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali habari Tanzania.

NA ABDI SULEIMAN.

CHAMA cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET), kimewataka watanzania kutokukata miti ovyo ovyo, badala yake kupanda miti kwa wingi ili kuendelea kulinda misitu nchini.

Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi Mtendaji wa JET Tanzania John chikomo, katika taarifa yake kwa yombo vya habari na wadau wa mazingira hivi karibuni.

Alisema misitu ni uhai na uhai unapaswa kulindwa kwa gharama yoyote ile, na ili kufanikisha hilo kila Mtanzania anapaswa kubeba jukumu la kutokata miti na badala yake anatakiw akupanda miti zaidi.

“Hatuna budi kuipongeza Serikali zetu mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na wadau wa misitu kwa kuwa mstari wambele katika kulinda misitu yetu nchini,”alisema Mkurugenzi.

Aidha Mkurugenzi Chikomo, aliwashauri wanachama wa JET na waandishi wa habari nchini Tanzania kuwa mstari wambele katika kupanda miti na kuhamasisha upandaji wa miti ili kupunguza hewa chafu angani.

Alisema wakati umefika wa kutunza miti ili kushiriki mapambano dhidi ya changamoto ya mabadiliko ya Tabia nchi ambayo yanaendelea kuikumba dunia na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zinazoathiriwa na mabadiliko hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu Zanzibar Said Juma Said, alisema uchomaji moto unaathiri sana misitu, hivi karibuni zaidi ya hekta 69 za msitu wa hifadhi ya Ngezi Kisiwani Pemba zimeteketea kwa moto.

Alisema moto mara nyingi inasababisha na usimamizi mbovu wa sheria, kwani wale watu wanaokamatwa kuwa na viashiria vya moto tutaweza kupiga hatia, kwani moto ulioathiri msitu umetokana na wapikaji wa Gongo ndani yam situ huo.

“Hizi hekta 69 ni pesa nyingi na zinakazi kubwa kuzirudisha, kwa kupanda miti ili kuwa katika uasilia wake, hapo miti adimu imepotea, bionuai nao wamepote ni athari kubwa imepatikana,”alisema.

Akizungumzia juu ya bionuai, alisema kila siku kwenye misitu kunapatikana viumbe vipya ambavyo duniani haviko, hivyo ipo haja ya wananchi kuilinda misitu kwa hali yoyote.

Haya hivyo aliitaka jamii kusimamia sheria ipasavyo na wale wanaokamatwa kufikishwa katika vyombo vya sheria na sheria kuchukua hatua kwa wale wanaoharibu misitu.

MWISHO