NA ABDI SULEIMAN.
TAASISI ya Tanzania Center For Education, imesema lengo la kuwasili Kisiwani Pemba ni kuwahamasisha jinsi gani wanaweza kufaulu masomo yao, pamoja na kuwajengea uwezo na misingi ya njisi ya kuweza kujibu maswali katika mitihani yao ya Taifa.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Yusuf Ogutu, wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, mara baada ya kuzungumza na wanafuynzi kutoka Skuli mbali mbali huko ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chake Chake.
Alisema zoezi la kuhamaisha wanafunzi walilianza mwaka 2022, kwa kujenga wanafunzi katika uwelewa wa namna ya mitihani inavokuja, kuwahamaisha na kuwaonyesha muhtasari wa masomo yalivyo na kuwapatia muundo wa mitihani na isthali zinazotumika katika mitihani.
“hili linamjenga mtoto kujuwa mapema jinsi maswali yanavyo ulizwa na unatakiwa kujibu hivi na kujiamini ili kuhakikisha mambo yake yanakuwa sawa,”alisema.
Aidha alisema wanafunzi wanauwelewa wa kutosha na hamasa kubwa kutokana na juhudi wanazozifanya walimu, Pemba asili yake watoto kufaulu ni jambo la kawaida, ila changamoto za malezi na jamii zimetatiza kidogo.
Alifahamisha kwamba wao wamekuja kuwasaidia walimu katika sehemu ndogo tu ambayo wanafunzi wanaisahau mara kwa mara, huku akiwataka wazazi kuhakikisha wanashirikiana kikamilifu na walimu ili kuona wanafunzi wanapaswa daraja la kwanza katika mitihani yao ya taifa.
Hata hivyo alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, kwa kuunga mkono katika zoezi la uhamaishaji kwa wanafunzi juu ya kupatikana kwa daraja la kwanza katika mitihadi ya taifa ya Kidato cha nne na Sita Zanzibar.
Naye mwalimu Mkuu wa Skuli ya Secondari Fidel Castro Seif Hamad Halfan, alisema wamefarajika sana ujio wa taasisi hiyo, kwani miaka ya nyuma nafasi hiyo ilikua haipo na waliona changamoto zilizopo kwa wanafunzi wao juu ya ujibuji wamitihani na matokeo yao.
Alisema baaha ya ujio wa taasisi hiyo mwaka jana, matokeo yalikuwa mazuri na imepelekea uhamaishaji kwa wanafunzi kwa hali ya juu, na tayari wamejipanga kuhakikisha wanaondosha daraja la pili katika mitihani yao.
“Mwaka jana kidato cha sita yalikua bora zaidi, daraja la kwanza 53 na daraja la pili 83 na zilizobakia daraja la tatau katika wanafunzi 153, na kidato cha nne daraja la kwanza 48 na daraja la pili Tatu, ni matokeo ambayo hayajawahi kutokea tokea ilipoanzishwa skuli hiyo,”alisema.
Kwa upande wa mwalimu wa taaluma skuli hiyo Abrahman Ali Rashid, alisema jambo hilo ni zuri na faraja kubwa, hali ambayo inataka kuungwa mkono na taasisi nyengine zilizobakia.
Hata hivyo aliziomba taasisi mbali mbali kuelelekeza nguvu katika masuala ya elimu, kwani inaweza kulijenga taifa lililokuwa zuri na bora kwa vijana.
Mwakilishi kutoka PBZ Hassan Khamis Hamad, alisema PBZ inawajali zaidi vijana na Pemba fursa nyingi zipo kwa vijana ambazo tayari wameshaanza kuzifuata.
Aliwataka wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa umakini na kupata alama ya kwanza katika masomo yao, kwani suala la elimu ndio kitu cha msingi kwa wanafunzi.
Kwa upande wao wanafunzi wa skuli za Sekondari Kisiwani Pemba, wamesema wataendelea kuhamaisha wenzao ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita.
MWISHO