Thursday, February 27

KAMPENI YA MAMA SAMIA YA MSAADA WAKISHERIA YATAMBULISHWA PEMBA

OFISA kutoka Ofisi ya Rais, Katiba Sheria utumishi na Utawala Bora Ali Haji Hassan akitoa ufafanuzi wakati wa utambulisho wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Kwa wadau wa sheria Kisiwani Pemba huko katika Ukumbi wa Wizara ya Katiba na Sheria Gombani Chake Chake Pemba, (PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

OFISA Mdhamini wa Ofisi ya Rais, Katiba Sheria, utumishi na Utawala Bora Kisiwani Pemba Halima Khamis Ali akizungumza na wadau wa sheria wakati wa utambulisho wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia huko katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria Gombani Chake Chake Pemba, (PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)
AFISA Sheria kutoka Ofisi ya Rais, Katiba Sheria, utumishi na Utawala Bora Yusra Abdalla Said akitoa maelezo wakati wa utambulisho wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Kwa wadau wa sheria Kisiwani Pemba huko katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria Gombani Chake Chake Pemba, (PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)
OFISA Mdhamini wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, utumishi na Utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali ameeliza kuwa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia itaweza kuibua na kumaliza changamoto za Kisheria zilizopo katika jamii.
Halimaaliyasema hayo huko katika Ukumbi Mkutano wa Ofisi za Katiba na sheria Gombani Chake Chake Pemba wakati akifungua kikao Cha kutambusha Kampeni hiyo Kwa wadau mbali mbali wa sheria Kisiwani humo.
Alieleza kuwa katika jamii Kuna matatizo mengi ambayo yanatendeka, hivyo ana matumaini makubwa kuwa Kampeni hiyo itakuwa ni chachu ya kutatua migogoro iliyopo ndani ya jamii.
Aidha Ofisa huyo alifahamisha kuwa Kampeni hiyo utaweza kuboresha mifumo ya upatikanaji wa haki katika njia tofauti pamoja na kuimarisha mashirikiano Kwa wadau katika utoaji wa Msaada wa Kisheria pamoja na kuifanya jamii kujua haki na wajibu wao katika Nchi.
“Kampeni hii inakuja na mifumo tofauti ya kisheria ambayo itakwenda kusimamiwa na kuboreshwa Kwa namna tofauti,ambapo Kampeni hii itakuwa ni miaka mitatu (3) na tayari Ina mpango kazi wake,” alifahamisha Ofisa huyo.
Sambamba na hayo Halima alisema kuwa Kampeni hiyo itaweza kuwafanya wadau wote wa sheria kuifahamu, kuielewa,kuitambua na kuwa tayari katika kutekeleza Yale yote ambayo yamepangwa katika Kampeni hiyo.
“Ni matumaini yetu ndani ya miaka mitatu (3) ya utekelezaji wa Kampeni hii itakuwa imeibua mambo mengi lakini pia imemaliza na kutokomeza changamoto nyingi sana za ufikiwaji wa haki katika jamii yetu,” alisema Halima.
Mapema akifunga kikao hicho, Ofisa huyo aliwataka wadau hao kuwa mabalozi Kwa wengine ili kuona kuona Kampeni hiyo inafanikiwa.
“Katika jamii zetu Kuna changamoto nyingi sana,ikiwa wanawake wanadhalilishwa pamoja na mirathi, hivyo ni wajibu wetu tushirikiane pamoja Ili kuondoa matatizo hayo,” alisema Ofisa huyo.
Hata hivyo aliwataka wadau hao kushirikiana pamoja, kushauriana na kuungana mkono katika kuyaendeleza Yale yote ambayo Viongozi wao wameyaanzisha.
Akitoa ufafanuzi wa Kampeni hiyo, Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,utumishi na Utawala Bora Yusra Abdalla Said alieleza kuwa lengo Kuu la Kampeni hiyo ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki Kwa wote kupitia huduma ya Msaada wa Kisheria nchini.
Aidha Yusra alisema kuwa Kampeni hiyo inalenga kuongeza uelewa wa sheria na upatikanaji wa haki,mifumo ya utoaji wa haki, masuala ya kisheria na haki za binaadam Kwa kujumuisha jitihada za Serikali, asasi za kiraia na wadau wa maendeleo katika utoaji wa huduma Kwa wananchi.
“Kampeni hii imetokana na maono ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha mfumo wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi bila ya kusubiria kuziwakilisha  changamoto zao wakati wa ziara za Viongozi wa kitaifa,” alisema Yusra.
“Kampeni hii inatarajia kuleta mabadiliko makubwa nchini katika maeneo tofauti ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma ya Msaada wa Kisheria Kwa wananchi wote,kuimarisha mfumo wa kutatua changamoto mbalimbali za Kisheria zinazowakumba wananchi kupitia mfumo wa utoaji haki,” alisema Yusra.
“Mbali na hayo lakini pia kuimarisha utaratibu wa huduma ya Msaada wa Kisheria, kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao pamoja na kuimarisha ushiriki wa wadau wote katika utoaji wa huduma ya Msaada wa Kisheria,”alifahamisha Ofisa huyo.
Nae mshiriki wa mkutano huo Massoud Ali Massoud kutoka Kamisheni ya Wakfu na Mali amana Pemba alieleza kuwa wameipokea vizuri Kampeni ya Mama Samia na kusema kuwa Serikali Ina mzuri ya kuboresha jamii yake katika nyanja hii ya sheria.
Aidha Massoud alifahamisha kuwa Kampeni hiyo itakuwa ni chachu na motisha Kwa Serikali ili kuweza kutatua migogoro iliyopo katika jamii.
“Ni kweli jamii zetu zimezungukwa na migogoro mingi katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo sehemu ya mirathi,migogoro ya ardhi pamoja na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia,” alieleza Massoud.
Sambamba na hayo Mshiriki huyo alisema kuwa Kampeni ya Mama Samia wanaiunga mkono kutokana na itakuja na morali ya utekelezaji mzuri ambao jamii itaelewa na kuweza kutatua changamoto zilizopo  ndani ya jamii ambapo lengo Hilo likifikiwa utaweza kuleta amani na utulivu ndani ya Nchi.
“Nina washauri wakuu wa Maidara na taasisi zote za Kiserikali na binafsi kuweza kuipokea Kampeni hiyo na kuifanyia kazi katika maeneo yao,” alisema Massoud.
Nae Zuhura Mussa kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Pemba alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan Kwa kuzindua Kampeni hiyo na kueleza kuwa wamefarajika sana kwani itaqasidia katika harakati zao za kila Siku.
Aidha Zuhura alimpongeza Dk, Samia Suluhu Hassan Kwa juhudi zake anazozichukua na kuamua kulitilia mkazo suala Hilo kwani ndio nguvu kazi ya taifa.
            MWISHO.