Saturday, December 28

KAMISHENI ya Utalii Zanzibar kumfariji mwekezaji wa hoteli ya kitalii ya EMERALD BAY  Chokocho Mkoani.

NA ABDI SULEIMAN.

KAMISHENI ya Utalii Zanzibar imesema ipo tayari kumsaidia mwekezaji wa hoteli ya kitalii ya EMERALD BAY ya Chokocho Mkoani, ili kuona hoteli hiyo inasimama na kurudi kufanya kazi zake.

Hoteli hiyo iliungua moto Machi 19 mwaka huu majira ya saa sita za mchana na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo ndani, huku chanzo cha moto huo ikidaiwa ni hitilafu ya Umeme.

Kamisheni imesema iwapo mwekezaji huyo atahitaji msaada kutoka serikalini, basi kamisheni ipo tayari kwani mwekezahi huyo alikua ameshakata leseni yake ya biashara kwa mwaka 2023.

Hayo yameelezwa na katibu mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Hafsa Hassan Mbamba, mara baada ya kukagua na kuangalia Hoteli ya EMERALD Bay ya Chokocho Wilaya ya Mkoani, iliyoteketea kwa moto yote.

Alisema hoteli hiyo imeunguka kwa asilimia 50% kwani kwa sasa limebaki jengo tupu hakuna chengine kilichobakia, huku akiwataka wafanyakazi na watendaji wa hoteli hiyo kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu kwao.

“Kakweli hasara kubwa imepatikana, vijana waliokuwa wakitegemea kupata riski zao hoteli hapo sasa nao hawanakazi, ikizingatiwa skukuu imeshakaribi ni jambo linalohuzunisha,”alisema.

Aidha alimuahidi msimamizi wa hoteli hiyo, kuwa leseni yao ya biashara waliokata itasogezwa mbele mpaka pale watakapofanya matengenezo upya na kuanza utoaji wa huduma na leseni itafanya kazi.

Hata hivyo aliwashauri wawezekazaji wa mahoteli ya kitalii, kwa sasa wakati wa kuezeka hoteli zao kuiga mfano wa hoteli zilizoko Stone Town, ambazo zimetenganishwa dari na paa kwa lengo la kuepuka athari za moto.

Naye msimamizi wa hoteli hiyo Ame Vuai Shein, alisema chanzo cha moto huo ni hitilafu za umeme, ambazo zilianza katika sehemu ya juu na kupelekea kuteketea kabisa kwa hoteli hiyo.

“baada ya kuona moto tulianza kuzima kwa kutumia maji ya ndoo, lakini siku hiyo kulikua na upepo mwingi moto uliweza kutushinda na kuungza hoteli yote,”alisema.

Alisema jambo kubwa siku hiyo ndio walikuwa na oda ya wageni 14 hotelini hapo, lakini kabla ya kushuka ndege waliwapeleka moja kwa moja hoteli ya mkoni kwa malazi, chakula wakiwahudumia wao.

Hata hivyo alisema mpaka sasa bado hasara yote haijajulikana, kwani wanaendelea kufikiria baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani, lakini tayari wameshawasilisha barua zao kwa taasisi mbali mbali za serikali katika suala zima la  kodi.

Watendaji wa kamisheni ya utalii zanzibar wakiongozwa na katibu matendaji wa kamisheni hiyo, walitembelea msitu wa hifadhi ya jamii micheweni na kumfariji mmiliki wa hoteli iliyoteketea kwa moto.

MWISHO