Sunday, December 29

KMKM wapo tayari kwa utafutaji wa mji wa karne ya kwanza.

NA ABDI SULEIMAN.

MKUU wa kikosi maalumu cha kuzuwia magendo Zanzibar KMKM Komodoo Azana Hassan Msingiri, amesema sasa wakati umefika kwa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba, kuwaruhusu kukamilisha jukumu la utafutaji wa mji wa karne ya kwanza ambao kwa sasa umeshaliwa na maji ya bahari.

Alisema kutokana na uwezo wa uwezo wa wazamiaji wao na vifaa vya kisasa walivyonavyo vya kisasa, wameweza kuuona baadhi ya vitu ikiwemo mawe makubwa chini ya bahari.

Msingiri alifahamisha kwa mji huo wa karne ya kwanza kwa sasa uko umbali wa mita 20 chini ya bahari, hivyo watahakikisha vitu vilivyoko chini vinaonekana kupitia vifaa vya kiasa, huku akiyomba Wizara kutokuruhusu kutumia wataalamu kutoka nje ya nchi.

“Tunapotumia wataalamu kutoka nje ya nchi gharama kubwa zinakuwa zinatumika, lakini sisi KMKM bahari ndio pori letu tunaloringia kwa kila kitu,”alisema.

Alifahamisha kwamba kuna mazingira ya kuonekana mabaki ya mji wa karene ya kwanza uliozama, ikiwemo mawe makubwa huko chini, kwa sasa eneo hilo limezungukwa na mchanga mwingi kutokana na hali ya hewa ya kaskazi.

Aidha alisema ikifika wakati wa hali ya hewa ya kusu, wanategemea kutakua na mabadiliko makubwa yatakayojitokeza katika eneo hilo kwa tameo la kuona kila kitu, kwani kutakuwa kuko wazi na watapata kugundua kile takiwa kukigundua.

Naye Luteni Kamanda Ameir Twalib Abdalla Mkuu wa kituo cha uokozi na uzamiaji Mkoani, ambaye aliongoza zoezi hilo la uzamiaji wa kutafuta mji wa karne ya kwanza ulizozamana chini ya bahari huko Mkumbuu, alisema wamefika sehemu na kukuta mawe makubwa ila kwa sasa yameanza kufukiwa na mchanga kutokana na hali ya hewa ilivyo.

Alisema kipindi cha kusi sehemu hiyo itakuw aipo wazai na wataweza kwenda kuona kila kitu kwa uhalisia, chamsingi ni kuhakikiwa wanaongeza vifaa ili waweze kugundua walichotakiwa na serikali.

“Baada ya mwezi mmoja au miwili mbele kipindi cha kusi, mchanga utakua umejiondoa katika sehemu husuika na tutaweza kuona kila kitu kilivyokua wa uwazi wake,”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Makumbusho na mambo ya kale Pemba Khamis Ali Juma, alisema wataendelea kuwatumia watafiti wazalendo katika tafiti zao mbali mbali, ambao KMKM imeonyesha uwezo mkubw akwa upande wa baharini.

Alisema katika hatua ya kwanz awameweza kupata kitu kama nanga katika aneo la mji huo wa kwanza, huku wakiahidi kupata vitu zaidi baada ya miezi miwili hali ya hewa itakapokuw aimebadilika.

Hata hivyo ambpongeza Komodoo Msingiri, kwa kuweza kuongeoza zoezi hilo la kuutafuta mji wa karne ya kwanza ambao kwa sasa umezama bahari.

MWISHO