Monday, November 25

DINI isiwe kikwazo kuhamsisha jamii juu ya suala zima la umuhimu wa amani nchini.-Profesa Ziddy

MHADHIRI wa chuo kikuu cha Zanzibar SUZA na Mwezeshaji wa mafunzo ya Vijana na Wazee Profesa Issa Ziddy, akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa vijana na wazee kupitia mradi wa amani na Maendeleo wa vijana na wanawake, unaotekelezwa na NCA, ZANZIC,ELCT-ND kwa ufadhili wa ubalozi wa Norway.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

NA ABDI SULEIMAN.

MKUFUNZI wa Masuala ya Amani Zanzibar Profesa Issa Haji Ziddy, amesema dini isiwe kikwazo katika kuhamaisha jamii juu ya suala zima la kujuwa umuhimu wa amani nchini.

Alisema suala la amani litaendelea kuwa muhimu katika nchi yoyote ile duniani, hivyo wananchi wanapaswa kutambua tahamani ya amani hiyo.

Akitoa mafunzo ya siku mbili kwa wadau wa masuala ya amani, mkutano uliiofanyika mjini chake chake kupitia mradi wa Amani na Maendeleo kwa Vijana na wanawake unaotekelezwa kwa pamoja na NCA, ZANZIC, ELECT-ND na kufadhiliwa na Ubalozi wa Norway.

Alisema ipo haja ya wananchi kuelimishwa katika suala zima la maendeleo, bila ya kujali dini, rangi au kabila, huku mashirikiano yakihitaji ili kufikia malengo.

Aidha alisema upo umuhimu mkubwa wa jamii kujitoa katika suala la kuhakikisha maendeleo yanapatikana, umoja na mshikamano ndio kitu muhimu cha kufikisha maendeleo ya nchini.

“Tunapokua wa maoja katika kila jambo uchumi utakua, maendeleo yatapatikana, upendo utaengelezaka,tuendeleee kuelimisha jamii katika suala zima la kuwa wamoja na kudumisha amani ya nchi,”alisema.

Kwa upande wake mchungaji Benjamini Kisaga, kutoka taasisi ya dini Mbali mbali Pemba alisema ipo haja kwa wazazi kushirikiana na serikali katika suala zima la malezi ya vijana wao, ili kuweza kuwa na vijana bora waliofundika.

Alisema taasisi yao imekua mstari wambele katika kusaidia vijana kupitia shuhuli mbali mbali za kilimo na ufugaji, ambapo huanza kwa kuawapatia mtaji kwa upande wa kilimo na ufugaji.

Naye mratibu wa mradi wa Amani na Maendeleo wa Vijana na wanawake Pemba Hidaya Dude, aliwataka washiriki kufahamua kwamba kila mtu na dini yake na mkutano huo sio kwa hubiri ya dini bali ni masuala ya maendeleo.,

Alisema katika suala la makatazo kuunganishe nguvu za pamoja, ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa, ikiwemo kutumika kwa aya za Qurani katika harakati zote za kuelimisha jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya Dini mbali mbali Pemba Shekhe Yussuf Abdalla, alisema dini zote zinakataza juu ya suala la liwati, hivyo ipo haja kwa viongozi hao kuhakikisha wanakemea kwa nguvu zao zote suala la ndoa za jinsia moja.

Naye Seif Haji Omar alisema suala kubwa ni maendeleo kwa vijana pamoja na vijana wenyewe kuwa na utayari pale wanapopatiwa mafunzo na mitaji kuhakikisha wanazalisho kilicho bora.

MWISHO