Monday, November 25

BINGWA mtetezi wa Intarfaith Amani Cup 2022 atetea kombe.

NA SAID ABRAHMAN.

 

BINGWA mtetezi wa Kombe la ‘Ujirani Mwema” Intarfaith Amani Cup 2022, timu ya Makoongwe ya Wilaya ya Mkoani imeweza kuendeleza ubingwa wake, baada ya kuifunga timu ya Wilaya ya Chake Chake Kwa mabao 2-0.

 

Katika mchezo ambao ulichezwa katika Kiwanja Cha Makombeni Wilaya ya Mkoani majira ya saa 10:00 za jioni, unaojulikana kama msafara wa Vijana wenye lengo la kuhamasisha Amani na Utengemano wa jamii ‘’Amani Yetu, Kesho Yangu’’.

 

Goli la kwanza la Makombeni liliwekwa kimiani mnamo dakika ya 35 ya mchezo huo na mchezaji Mohammed Juma baada ya kuwatoka walinzi wa timu ya Wilaya ya Chake Chake.

 

Kuingia Kwa bao hilo Chake Chake walijitutumua ili kutaka kusawazisha makosa yao lakini Hadi kipindi Cha kwanza kinamalizika Makombeni moja huku Chake Chake bila.

 

Kipindi Cha pili kilianza kwa taratibu kwa kila timu kusoma mchezo wa mwenzake, huku timu ya Wilaya ya Mkoani ikidhibiti na kulinda zaidi goli lao.

 

Waswahili wanasema ‘mgagaa na Pwani Hali Chakula kitupu’ kwani mnamo dakika ya 70 Issa Haji Khamis wa Makoongwe aliweza kuwahakikishia wapenzi wa timu yao baada ya kufunga ya kufunga bao la 2.

 

Hadi mwisho wa mchezo huo Wilaya ya Mkoani 2-0, huku fainali ya Intarfaith Amani Cup 2023, inatarajiwa kuchezwa baina ya Wilaya ya Wete na Micheweni.

 

MWISHO