Thursday, November 14

NMB yakabidhi bati yenye thamani ya Milioni 12 Maandalizi Machomanne.

NA ABDI SULEIMAN.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba  Mattar Zahor Massoud, amesema benk ya NMB nimoja ya benk zilizo mstari wa mbele katika kusaidia Serikali huduma mbali mbali kimaendeleo.

Alisema NBM tayari imeshasaidia mambo mengi ndani ya mkoa wa kusini Pemba, katika Nyanja za kielimu, afya na hata kwenye michezo na matamasha mbali mbali ya serikali.

Mkuu huyo wa mkoa aliyaeleza hayo katika hafla ya makabidhiano ya bati 260 zenye thamani ya Milioni 12 kutoka wa benk ya NMB kwa ajili ya skuli ya maandalizi Machomanne Wilaya ya Chake Chake.

Mkuu huyo aliishukuru NMB kwa jitihada zake za kusaidia jamii katika Nyanja mbali mbali, kwani fedha walizotenga kwa mwaka huu bilioni 6.2 sio fedha kidogo katika kusaidia Sekta ya elimu, Afya na Mazingira.

“NMB ni moja ya benk ya kizalendo hapa nchini na imekua benk ya mfano katika kusaidia jamii, imeshaka nafasi ya kwanza mara kadhaa kile wanachokipata wanakirudisha kwa jamii,”alisema.

Aidha alizitaka baadhi ya Taasisi za kifedha kuhakikisha wanafuata nyao za benk hiyo katika kusaidia jamii, kwani wananchi wanahitaji mambo mengi.

Akizungumzia seula la Elimu, Mkuu huyo aliwashukuru walimu wa skuli hiyo katika jitihada zao za kuimarisha maendeleo ya skuli hiyo, huku akiahidi kuifanyia kazi changamoto ya uzio kwa skuli hiyo ambao utawafanya wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.

Alisema serikali inaendelea na mikakati yake ya kuimarisha miundombinu ya elimu, kwani mwaka huu imekusudia kujenga skuli kadhaa za ghorofa kwenye maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba.

“Sote ni mashahidi NMB imetukabidhi bati 260 sio bati kidogo hizi zitatumika katika maeneo yetu ya skuli tutakayojenga, huu sio msaada modogo kwetu,”alisema.

Hata hivyo alisema bila ya elimu hakuna mipango yoyote ya maendeleo yatakayofanyika, hiyo aliwataka walimu kuendelea kuwasomesha wanafunzi hao, ili kufikia ndoto zao za kimaendele kuwa wataalamu wazuri wabaadae.

Kwa upande wake Meneja wa Biashara wa NMB Kanda ya Zanzibar Naima Said Shaame, aliwashukuru walimu wa skuli ya maandalizi machomanne kuona benk ya NMB ni sehemu salama pakufikisha changamoto zao na kuweza kutatuliwa kwa wakati mkuwafaka.

Alisema NMB imepokea maombi mengi lakini suala la elimu, ndio kipaombele chao mwaka 2023 imetenga bilioni 6.2 kwa ajili ya elimu, Afya na Mazingira.

“Kwa sasa NMB inamawakala zaidi ya elfu 20 Tanzania nzima, Matawi 220 na ATM zaidi ya 780, mikakati yetu ni kuongeza tawi kwa upande wa Wete,”alisema.

Aidha aliwataka wananchi kuendelea kuiamini benk hiyo kwa kuweka amana zao mbali mbali, pamoja na kunufaika na fursa zinazotolewa na benk hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Msifu Nassor Hamad, aliwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia changamoto mbali mbali zinazoikabili skuli hiyo.

Mapema akisoma risala ya skuli hiyo Hadija Abrahman, alisema skuli hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uzio, uhaba wa walimu, uhaba wa madarasa kutokana na wingi wa wanafunzi kwani skuli ina wanafunzi 452 na walimu sita na madarasa matano ya kusomea.

MWISHO