Ikiwa imesalia miaka miwili wananchi wa Tanzania kutekeleza haki yao ya kikatiba kuchagua na kuchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu mwaka 2025 Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amewataka wanawake wenye nia za kugombea kutokubali kutumiwa na wenye ajenda zao, zikiwemo za kukwamisha wanawake kutoshika nafasi za uongozi.
Aliyasema hayo wakati alipokua akizungumza na wanawake kutoka vyama mbali mbali vya siasa Zanzibar katika ofisi za chama hicho Tunguu Wilaya ya kati Unguja.
Alisema licha ya kuwa Zanzibar ina idadi kubwa ya wanawake wengi zaidi lakini kwa mshangao mkubwa bado wanawake hao hawapati nafasi ya kuchaguliwa kutokana na kasoro mbali mbali zikiwemo za mitazamo hasi iliokua ikitawala kwenye jamii.
Alieleza kuwa ili wanawake welio wengi waweze kufanikiwa kwenye uchaguzi huo hawana budi wao wenyewe kushikana na kuwa wamoja zaidi na kukataa kabisa kubaguliwa.
Akitoa ushuhuda wa mafanikio mwanamke aliewahi kuwa mgombea katika na kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi kwa nafaisi ya uakilishi jimbo la Magomeni mwaka 1995.Hafsa Said Khamis amesema mafanikio ya kuchaguliwa kuwa mgombea kwenye wakati mgumu zaidi ambao wanawake hawakuweza kupaza sauti zao,kwenye mazingira ambayo yeye alithubutu.
‘’Kila mmoja anafahamu hapa kuwa tulipotoka kulikua kubaya zaidi wanawake wengi walibaki kuwa watumwa kwenye nafasi za uongozi lakini leo hii wengi wenu munajitokeza hadharani kutaka uongozi’’aliongezea.
Akieleza kuhusu siri ya mafanikio yake, amesema ni kutokana na kujijengea utaratibu wa kupenda watu wa rika zote bila ya kuwabagua wengine kwa sababu ya kutofautiana kwao kisiasa.
‘’Mimi nilikua karibu sana na watu na watu wenyewe ndio walikuja kuniambia ningie kwenye siasa nakumbuka Baba yangu nilipokwenda kumuambia alishangaa na kuona siwezi’’lakini nilithubutu.
Kuhusu maendeleo yake aliowahi kufanya akiwa kama kiongozi wa jimbo,amesema ni pamoja na kufanikiwa kusimamia ujenzi wa skuli ambayo ilikua na madarasa manne na mpaka leo hii ipo na wananfunzi wanaendelea kupata elimu.
*Mwisho*