Friday, November 15

CP ZANZIBAR KUSIMAMIA HAKI ZA BINAADAMU

NA OMAR HASSAN – ZANZIBAR .
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad ameahidi kuwahimiza Askari wa Jeshi la Polisi kuendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za Nchi na za Jeshi hilo ili wasivunje haki za Binaadamu.
Kamishna Hamad ametoa ahadi hiyo mara baada ya Tume ya haki za Bidaadamu kutoa mafunzo ya haki za binaadamu kwa maafisa wa Polisi wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa watendaji wa Jeshi hilo na kwamba watatumia Wakaguzi wa Shehia kutoa Elimu kwa wananchi kwa vile wananchi wengi hawazijui haki zao.
Nae Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania Khatib Mwinyi Chande amesema Tume hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuimarisha utendaji unaozingatia haki na utawala bora.