Thursday, January 16

Maandalizi Machomanne, waomba wadau mbali mbali  kuwasaidia ujenzi wa ukuta katika skuli hiyo ili kulinda afya za wanafunzi wanaosoma skulini hapo

NA ABDI SULEIMAN.

UONGOZI wa Skuli ya Maandalizi Machomanne, umewaomba wadau mbali mbali wa maendeleo kuwasaidia ujenzi wa ukuta katika skuli hiyo ili kulinda afya za wanafunzi wanaosoma skulini hapo.

Uongozi huo umesema hali imekuja kufuatia kutolewa kwa mifereji katika vyoo vyao vya kiasasa na watu wasiojulikana, pamoja na kutupwa ndani hodhi la maji ya kunywa mfuko wa kinyesi cha binaadamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mwalimu mkuu wa skuli hiyo Msifu Nassor Hamad, alisema maji hayo tayari walishatumia kwa mrefu na wanafunzi skulini hapo, bila ya kujua kilichokuwemo ndani.

“Tuliamua kumtafuta fundi kwa ajili kuja kulisafisha fundi baada ya kupanda juu na kuchungulia alikuta kinyesi kikiwa kimetapakaa na kutuaria na sisi tukaamua kuyatoa maji yote, ili kusafishwa hapo awali tushatumia kwa muda mrefu lakini,”alisema.

Alisema kutokana na skuli yao kukosa uzio maalumu uliozunguka, matukio kama hayo yameanza kujitokeza hali inayohatarisha maisha ya wanafunzi wa skuli hiyo.

Akizungumzia tukio la kutolewa mifereji katika vyoo, alisema sio kitendo kizuri wala cha kiungwa kufanyika katika skuli hiyo, kwani mifereji hiyo wanaotumia ni watoto wadogo.

Aidha aliwataka wadau mbali mbali, mabenk, viongozi wa Serikali na majimbo kujitokeza kusaidia changamoto za skuli hiyo, ili wanafunzi waweze kusoma kwa amani.

Mwalimu huyo alisema kilio hicho tayari aliashakifikisha kwa viongpozi wa Jimbo hilo Mwakilishi, Mbunge na diwania, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kusaidia kwa sasa.

Mjumbe kutoka kamati ya skuli hiyo Abdalla Mohamed, alisema tayari uongozi wa skuli umeshalifikisha kwa wazazi suala hilo juu ya kujenga uzio skulini hapo, ili kulinda mali za skuli na afya za wanafunzi.

alisema baada ya wanafunzi kutoka eneo hilo linakua wazi, linatumiwa na vijana tafauti waliwemo wavutaji wa sigara na mambo mengine, hivyo litakapoekewa uzito litakua katika mikono salama muda wote.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud hivi karibuni katika hfla ya kupokea bati za skuli hiyo, alimuahidi mwalimu mkuu huyo kuchangia mifukpo 30 ya saruji wakati ujenzi utakapoanza.

Skuli ya maandalizi Machomanne ina wanafunzi 452 na walimu sita na madarasa matano ya kusomea.

MWISHO