Thursday, January 16

Mashabiki wa Yanga wapongezwa Pemba.

NA HANIFA SALIM.

MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba (Pemba Press Club) Bakar Mussa Juma, amewapongeza mashabiki wa timu ya Yanga nchini kwa hatua waliofikia ya fainali ya Kombe la Shirikisho barani Africa.

Mwenyekiti huyo alisema timu hiyo imeipa haeshima kubwa Tanzania, kutokana na kutinga kwao Fainali ya mashindano hayo, hali itakayovifanya baadhi ya vilabu vya Africa kuogopa Timu za Tanzania.

Bakar ambaye ni shabiki Mkubwa wa Timu ya Simba Kisiwani hapa, alilazimika kuwapongeza watani wao wa jadi Yanga kwa ngazi waliofikia.

“Sasa Soka la Tanzania limeanza kuimarika na kukua kwa kaisi kikubwa, Timu ya samba imeshafikia hatua ya fainali kama hii miaka kadhaa iliyopita, pia imeshirikia Robo fainali ya klabu bingwa mara nyingi, mpira kweli umakua na tunaendelea kujijenga kama soka letu kubwa,”alisema.

Hata hivyo mwenyekiti huyo, aliwataka mashabiki wenzake wa simba sasa kuungana na kuwa kitu kimoja pale timu zao zinaposhirikia mashindano ya kimataifa kwa kuziunga mkono kwa pamoja.

Wakati huo huo nae Shabiki wa Timu ya Yanga Kisiwani Hapa, Hassan Khamis Othman aligawa halua kwa wadau mbali mbali michezo kufuatia timu yake kutinga hatua ya fainali ya kombe la shirikisho.

Timu ya Yanga imefanikiwa kuifunga timu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini Bbao 2-1 katika mchezo wa marudio uliopigwa katika uwanja wa Royal Bafokeng.

MWISHO