Na Maelezo.
Mawakili na Wanasheria wamehimizwa kujiendeleza kielimu katika fani zao ili kuwa na taaluma zaidi ya kuendesha kesi mahakamani.
Hayo yamesemwa na Rais wa Chama cha wanasheria Zanzibar Slim Said Abdallah wakati alipokua akifungua Mhadhara (Mafunzo) wa Sheria kuhusu Uwasilishaji wa Hoja mbele ya Mahakama(SUBMISSION) katika Ukumbi wa ZSSF Kariakoo.
Amesema wakili lazima awe na taaluma na ujunzi wa hali ya juu katika kuendesha kesi mahakamani kwa kutumia kanuni na sheria za mawakili ili jamii iweze kumuamini na kumkubali katika utekelezaji wa majukumu yake , na kuongeza kuwa endapo wakili atakosa utaalamu huo hutaweza kufanya kazi zake kwa ufanisi .
Aidha amefahamisha kuwa lengo la muhadhara huo ni kuwajengea uwezo mahakimu,majaji, mawakili na makadhi katika utendaji wao ili kuweza kwasilisha kesi katika mahakama.
Amefafanua kuwa kazi ya uwakili imegawika katika sehemu mbili ikiwemo kukushanya data sehemu tofauti (Research) na kuziwasilisha kwa ufanisi ili ziweze kufahamika.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wahusika katika kada ya sheria kwa kuwawezesha mawakili kufanya vizuri katika kazi zao na kuleta tija kwa wanafunzi wa Skuli hiyo hadi kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Nae hakimu wa Serikali Zubeir Ali Awamu amesema kuwa mafunzo hayo yataleta faida kubwa hasa kwa makadhi kwani wameweza kupata elimu kuhusu uwasilishaji katika mahakama jambo ambalo litaondosha usumbufu katika kazi.
Akizungumzia kuhusu uwajibishwaji Zubeir amefahamisha kuwa mwanamke anaweza kushiriki katika kesi ikiwa kulikua na kikundi cha watu fulani na akashuhudia tukio husika hivyo ipo haja kwa watoto wa kike kuwajibishwa ikiwa amefanya kosa .
Amefafanua kuwa mtoto wa kike anaweza kuwajibishwa ijapokuwa adhabu haitofanana na mwanamme kwani kufanyiwa hivyo ataweza kujikinga na kujiepusha na vitendo viovu jambo ambalo litasaidia kujilinda kuingia katika vitendo hivyo.
Hata hivyo Zubeir amewataka Mawakili wenzake wa Serikali na wakujitegemea kuendelea kujifunza zaidi ili kukabiliana na kesi ya aina na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Akiwasilisha Mada ya Uwasilishwaji Hoja mbele ya Mahakama Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof: John Ruhangisa amesema kuwa wakili mzuri lazima awe na elimu ya kutosha na kufahamika wakati anapowasilisha kazi zake .
Mafunzo ya hayo yameandaliwa na Skuli ya Sheria Zanzibar na kuwashirikisha wadau mbalimali wakiwemo Majai, Mahakimu, Mawakili, Makadhi na Wanafunzi wa Skuli hiyo.