UTPC jana imeendesha kikao kazi maalumu na waratibu wa klabu za waandishi wa habari nchini kikiwa na lengo la kufanya ufuatiliaji wa mambo yaliyokubaliwa katika vikao vilivyopita ambayo kimsingi ni kuboresha utendaji wa klabu za waandishi wa habari ili kufikia dira ya kuitoa UTPC mahali pazuri na kuipeleka pazuri zaidi (Moving UTPC from Good to Great)
Pamoja na mambo mengine, kikao kazi hicho kilijadili shughuli zilitelelezwa na klabu za waandishi wa habari nchini katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Mei 2023 lakini pia kueleza mipango iliyopo kwa kipindi cha mwezi Juni 2023.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa UTPC Bw. @kennethsimbaya ametumia fursa hiyo kuziomba Klabu za waandishi wa habari kuwasimamia vizuri waandishi wa habari ili kutimiza adhima ya vyombo vya habari ya kuwa sauti ya wasiyo kuwa na sauti badala ya kuwa waandishi wa matukio tu.
Naye Ofisa Programu anayesimamia Utawala na Maendeleo ya Klabu, Bi. @hildakileo1 amesisitiza uwajibikaji na kuzingatia weledi katika kazi kwa waratibu wa klabu ili kuleta tija na kuchochea ustawi wa klabu za waandishi wa habari nchini.
Jumla ya waratibu 28 kutoka klabu zote bara na visiwani wamehudhuria kikao hicho ambacho kimeendeshwa kwa njia ya mtandao (Zoom).