Saturday, February 22

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar awapa neno wakulima wa miradi ya viungo,

NA ABDI SULEIMAN.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Dk.Omor Ali Ameir, amewataka wakulima walio katika progamu ya miradi ya viungo, kuhakikisha wanakuwa na mipango ambayo itawasaidia mara baada ya muda ya miradi hiyo kumalizika.

Alisema Programu hizo zinawawezesha wakulima hao, kupitia Jumuiya za asasi za kiraia chini ya udhadhili wa Umoja wa Ulaya(EU) ni mkubwa, na endapo zitasimamiwa vyema baada ya mradi kumalizika basi wakulima watakuwa wamepata mahali pa kushika.

Naibu Katibu Mkuu aliyesema hayo, kwa nyakati tofauti katika ziara maalum ya kutembelea miradi ya kilimo cha viungo na mboga mboga, kwa wakulima wa kisiwani Pemba lengo ikiwa ni kujionea maendeleo ya wakulima hao.

Alisema lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ni kushirikiana na mashirika yanayoendesha mipango hiyo, na kuona kunakuwepo na mageuzi makubwa kwenye kilimo cha viungo, mboga na kuongeza tija na kipato kwa mkulima mmoja mmoja au vikundi vyao.

Hata hivyo Naibu Katibu Dk.Omar, alieleza kufurahishwa kwake na hatua iliyofikiwa na wakulima hao, katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora, ambazo zinawaongezea kipato wakulima kinachowasaidia kujikimu kimaisha na kusaidia kutoa ajira kwa watu wengine.

“Hatua muliofikia ni kubwa kweli hichi kilimo chja  viungo kama utakithamini na kukijali basi kitakufikisha sehemu kubwa sana katika maisha,”alisema.

Kwa upande wake mshauri wa Umoja wa Ulaya katika miradi hiyo ya Viungo Anna Costantine, alisema matumaini yake na umoja wa Ulaya kupitia miradi hiyo, kumeanza kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wakulima kwa kuongeza tija, katika uzalishaji na kuweza kumudu changamoto zilizokuwa zikiwakumbwa huko nyuma.

“Naamini changamoto zile za ukosefu wa maji, wadudu waharibifu na nyenginezo kwa kiasi zimepungua kwenu wakulima, ni mmeongeza ubora katika uzalishaji na kupata masoko ya bidhaa hizi za viungo na mazao mengine yatokanayo na kilimo,”alisema.

Wakiwa katika shamba la Mapungwi Cooperative Group huko Kangagani Wilaya ya Wete, ujumbe huo uliweza kujionea maendeleo ya uzalishaji kwa wanakikundi hicho ambapo Katibu wa Kikundi hicho Ali Khamis Kombo alitaja baadhi ya mafanikio na Changamoto zao.

Alisema baadhi ya mafanikio waliyoapata ni pamoja na kuongezeka kwa mapato, yaliyotokana na kilimo chao kwani msimu huu waliweza kulima vitunguu robo eka, na kufanikiwa kupata jumla ya shilingi milioni tatu, nyanya milioni 4.5, huku matikiti yakiwaingizia milioni 3.5.

Aidha alizitaja baadhi ya changamoto kubwa kwa sasa, ni maji jambo ambalo yamekuwa ni shida katika umwagiliaji na kutegemea mvua, ambapo TAHA wamekuwa bega kwa bega katika kuwaelekeza na  wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao yao.

Kwa upande wake Mkulima wa mananasi, tungule, maboga na matikiti Salum Issa Moh`d wa Wambaa, alisema namna walivyopiga hatua katika uzalishaji wao, kwani wamepata mashirikiano ya kutosha kwa wasimamizi Pemba Community Forest.

“Kwa sasa changamoto kubwa kwetu ni kutofikiwa na huduma ya umeme, lakini tumeshakamilisha taratibu zote kilichabaki ni ZECO kujakutuungia<alisema.

Ujumbe huyo ulitembelea maeneo mbali mbali ya wakulima wa viungo na mboga mboga kisiwani Pemba, ikiwa ni Pamoja na Kangagani -Wete, Mjini Ole-Chake Chake, Wambaa na Mkanyageni katika Wilaya ya Mkoani pamoja na Skuli ya Msingi ya Pembeni Chake Chake.

MWISHO