Saturday, December 28

Dk. Mwinyi amefanya mazungumzo na Mkuu wa Taasisi ya bahari ya Korea, Dk. Kim Jong -Deog  Ikulu, Zanzibar

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Serikali ya Korea kwa jitihada zake za kuendelea kuiunga mkono Tanzania ikiwemo Zanzibar kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo hasa sekta ya Uchumi Buluu.*
Dk. Mwinyi ametoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Mkuu wa Taasisi ya bahari ya Korea, Dk. Kim Jong -Deog aliyefika kwa mazungumzo pamoja na kumualika kongamano kubwa la uvuvi la Afrika, litakalohusisha Taasisi ya bahari ya Korea na nchi zote za Ukanda wa bahari ya Hindi.
Alisema, anaamini mkutano huo utawajengea uwezo wananchi wengi zaidi katika kujikomboa na kujifunza mengi yatakayotokana na mkutano huo na kueleza kuwa ni fursa nzuri kwa ustawi wa sekta ya uvuvi Zanzibar.
Alisema, Uvuvi ni sekta kiongozi baada ya Utalii unaochangia asilimia 30 ya uchumi wa Zanzibar nakuongeza kuwa sekta mbili hizo zinamchango mkubwa kwa maendeleo ya Zanzibar.
Alisema anaamini mkutano huo utawajengea uwezo wananchi wengi zaidi katika kujikomboa na kujifunza mengi yatakayotokana na mkutano huo na kueleza kuwa ni fursa nzuri kwa usatawi wa sekta ya uvuvi Zanzibar.
Alisema, Uvuvi ni sekta kiongozi baada ya Utalii unaochangia asilimia 30 ya uchumi wa Zanzibar na kuongeza kuwa sekta mbili hizo zinamchango mkubwa kwa maendeleo ya Zanzibar.
Akizungumzia kilimo cha mwani, Rais Dk. Mwinyi aliueleza mgeni huyo kwamba asilimia kubwa ya jamii zinazoishi kwenye ukanda wa bahari hujishughulisha na kilimo cha mwani ambao wengi wao ni wanawake, hivyo alimueleza kwamba Serikali ndio yenye jukumu la kuwainua kiuchumi katika kuunga mkono jitihada zao.
Alisema, Korea inamchango mkubwa katika kuiunga mkono Tanzania ikiwemo Zanzibar hasa kwenye masuala ya maendeleo ya uvuvi, ambapo alieleza wanashirikiana kwenye maeneo tofauti ya uhusiano wao wa diplomasia.
Naye, Dk. Kim Jong – Deog alimueleza Dk. Mwinyi lengo la Kongamano hilo baina ya Korea na Afrika ni kuongeza Ushirikiano na kubadilishana uzoefu kwenye rasilimali za bahari ikiwemo sekta ya uvuvi.
Alisema, mkutano huo wa kimataifa utakua wa 9 pia ni kwanza kufanyika Afrika Mashariki, kupitia ukanda wa bahari ya Hindi, utajadili fursa na rasilimali za bahari zitakazoakisi azma ya zana nzima ya uchumi wa buluu nchini.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, alieambatana na ugeni huo kutoka Korea, Balozi, Togolani Edriss Mavura alimsifia Dk. Mwinyi, mafaniko makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Korea kupitia uchumi wa bahari pamoja na maendeleo ya viwanda vya kuchakata rasilimali na mazao ya maharini.
Alisema, licha ya Korea kupitia changamoto sawa kama Tanzania zinazotokana na sekta ya uvuvi na mazao ya baharini lakini kwa kiasi kikubwa Korea wamepiga hatua kimaendeleo kwenye maeneo hayo.
Alisema, Tanzania inamatarajio ya kujifunza mengi kutoka kwao na wamekua kwenye majadiliano na wawekezaji kwa kuonesha maeneo ya mbalimbali ya kuyafanyia kazi hasa kupitia sekta ya Uchumi wa Buluu na masuala mengine ya Utalii.
Pia balozi Togolani alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kuwa kinara kwenye sekta ya Uchumi wa Buluu ambae amefanikiwa kwa kiasi kikubwa ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake tokea alipokuja na sera hiyo mwaka 2020.
Alimweleza Dk. Mwinyi mara alipowasili Korea alizungumza na Serikali ya nchi hiyo mazuri yote yaliomo Tanzania ikiwemo Utalii, uvuvi pamoja na sekta kinara ya Uchumi wa buluuu na kuahidi kuwafututia wawekezaji wengi.
*IDARA YA MAWASILIANO – IKULU, ZANZIBAR*