Monday, November 25

16/06- SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.

Tarehe 16,Juni kila mwaka ni siku ya mtoto wa Afrika. Historia inaonesha kuwa tarehe kama hiyo mwaka 1976, maelfu ya watoto katika nchi ya Afrika Kusini walikusanyika katika mji wa Soweto kwa ajili ya maandamano yenye malengo ya kudai elimu bora.
Maandamano hayo yalipelekea mamia ya watoto kupigwa risasi na kuuliwa, huku watoto zaidi ya elfu moja kujeruhiwa.
Katika kuenzi michango ya watoto walioshiriki maandamano hayo.Umoja wa Afrika uliteua siku hiyo kuanzia mwaka 1991 kwa ajili ya kuwajengea uelewa wanajamii juu ya umuhimu wa elimu bora kwa watoto.
Kauli Mbiu ya Kimataifa ya siku ya mtoto wa Afrika kwa mwaka wa 2023,inalenga kuangalia haki za watoto katika mazingira ya kidigitali yaani “π™©π™π™š π™§π™žπ™œπ™π™© 𝙀𝙛 π˜Όπ™›π™§π™žπ™˜π™–π™£ π™˜π™π™žπ™‘π™™ π™žπ™£ π™©π™π™š π™™π™žπ™œπ™žπ™©π™–π™‘ π™šπ™£π™«π™žπ™§π™€π™£π™’π™šπ™£π™©.