Monday, November 25

Watendaji wa Mahkama Kisiwani Pemba watakiwa kujiepusha na Rushwa na uhujumu wa uchumi.

KHADIJA KOMBO-PEMBA.

 

Watendaji wa Mahakama Kisiwani Pemba wametakiwa   kufanyakazi kwa uadilifu na uwajibikaji kwani wao ndio tegemeo kubwa   la wananchi   katika kupata haki zao.

Akifungua warsha ya siku moja kwa Watendaji wa mahakama Kisiwani Pemba Jaji Mkaazi Pemba Mh. Ibrahim Mzee Ibrahim amesema watendaji hao ndio roho ya mahakama,   hivyo hawana budi kufanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa huku wakiwa tayari kukataa rushwa na uhujumu wa uchumi nchini.

Kwa upande wao washauri waelekezi Khamis Kombo Mohammed kutoka ZAECA na Suleiman Omar Suleiman   kutoka Chuo cha Utawala wa Umma wamesema  kuna baadhi ya watendaji ambao si waadilifu hivyo huchukulia nafasi zao kama njia ya kudai rushwa hivyo hakuna budi kubadilika ili kuondokana na vitendo hivyo ambavyo vinaathari kubwa ndani ya jamii.

Akifunga warsha hio Naibu Mrajis wa Mhakama Pemba Faraji Shomari Juma amesema  lengo kubwa la warsha hio ni kuwajengea uwezo watendaji wa mahakama ili waweze kuwajibika ipasavyo huku wakifanyakazi kwa uadilifu.

Warsha hio ya Siku moja imewashirikisha wafanyakazi wa Mahakama zote kisiwani Pemba zikiwemo wa za Mkoa Wilaya na Mahakama za Kadhi.

MWISHO.

 

ANGALIA VIDEO YA HABARI HII KWA KUBOFYA VIDEO  HAPO CHINI