Monday, November 25

HABARI PICHA: CYD yawapa mafunzo vijana Wilaya ya wete juu ya kudumisha Amani .

MKURUGENZI Mtendaji wa kituo cha majadiliano kwa vijana (CYD) Zanzibar, Hashim Pondeza akitoa maelezo mafupi juu ya mradi wa Dumisha Amani kwa Vijana 15 wa Wilaya ya Wete, Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa baraza la Mji Wete.
MWAKILISHI kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) Gamaliel Sunu, akitoa salamu za UNDP wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Mradi wa Dumisha Amani kwa 15 wa Wilaya ya Wete mradi wa Dumisha Amani Wilaya
MKUU wa Wilaya ya Wete Dkt.Hamadi Omar Bakari, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Vijana 15 kutoka Wilaya hiyo, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa Dumisha Amani ndani ya Wilaya hiyo mradi unaotekelezwa na taasisi ya CYD
MKURUGENZI Mtendaji wa kituo cha majadiliano kwa vijana (CYD) Zanzibar, Hashim Pondeza akimkabidhi kitini cha Vijana, Amani na Usalama Mkuu wa Wilaya ya Wete Dkt.Hamad Omar Bakar, kitini kinachozungumzia masuala la Vijana na Amani, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa Dumisha Amani mkutano uliofanyika Wete.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)