Saturday, December 28

MAPINDUZI YA MIUNDOMBINU YA UTALII KILWA KISIWANI YAWAACHA MIDOMO WAZI WATALII 120, TAWA SEA CRUISER YAWA GUMZO

Na. Beatus Maganja 
Hifadhi ya Magofu ya kale Kilwa Kisiwani na Songo Mnara imeendelea kuwa na mvuto mkubwa Kwa watalii wa ndani na wa nje kutokana na mapinduzi makubwa ya kimiundombinu yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi imara wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Juni 17, 2023 Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA imepokea jumla ya watalii 120 waliotembelea na kutalii katika Hifadhi ya Magofu ya kale Kilwa Kisiwani na kueleza kuridhishwa kwao na Utalii wa kutumia boti la Kisasa lenye kioo Maalum kinachomwezesha mtalii kuona viumbe hai vilivyopo chini ya bahari iliyozinduliwa mapema Mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa
Watalii hao wamesema matarajio yao yamefikiwa Kwa kiwango cha juu zaidi ya walivyofikiria awali kabla ya kufika katika hifadhi hiyo kutalii na kuliona boti hilo la Kisasa almaarufu “TAWA Sea Cruiser “
“Sikuwahi kufikiria kama Kuna boti ambalo lina kioo chini halafu unaweza kuona mpaka chini ya bahari, tumeona viumbe vingi sana ambavyo hatukufikiria kuviona ” alisema mtalii
TAWA inaendelea kuwahamasisha watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani kutembelea Hifadhi hiyo kujionea mapinduzi ya Utalii yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia wafurahie uzuri wa Utalii wa baharini, kiutamaduni na kihistoria