NA SAID ABRAHAMAN-PEMBA
WIZARA ya afya ya Zanzibar imesema kuwa kazi kubwa iliyonayo ni kuwapatia elimu wananchi juu ya maradhi yasioambukiza sambamba na kupunguza vifo vya akinamama na watoto.
Hayo yalielezwa na Ofisa Mdhamini wa Wizara ya afya Kisiwani Pemba Khamis Bilal Ali wakati akifungua mafunzo ya Siku mbili Kwa waandishi wa habari juu ya maradhi yasioambukiza huko katika Ukumbi wa hoteli ya Samail Gombani Chake Chake Pemba.
Bilali alibainisha kuwa katika Bajeti ya mwaka 2023/2023 ya Wizara ya afya ni kuona inapunguza Kwa asilimia kubwa wananchi wake Kwa kuwapatia elimu Ili kuweza kupunguza Kwa asilimia kubwa Kwa maradhi yasioambukiza.
“Nikipongeze Kitengo Cha maradhi yasioambukiza kutokana na kubwa inayofanya, tokea kuanzishwa kwake kwani kimekuwa kikifanya kazi kubwa ili kuona jamii iko katika Hali ya salama Kwa magonjwa hayo,” alieleza Ofisa huyo.
Sambamba na hayo Mdhamini huyo aliwataka waandishi wa habari hao kuitumia vyema elimu watakayoipata katika mafunzo hayo ili kuielimisha jamii juu ya maradhi hayo.
“Niwaombe ndugu waandishi wa habari elimu mutakayoipata katika mafunzo haya mukaitoe Kwa jamii ili iweze kutambua athari ya maradhi hayo,” alisema Ofisa huyo.
Mapema akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Dk, Husna Suleiman Juma alisema kuwa Kwa tathmini iliyotolewa na Shirika la afya duniani (WHO) imeweza kuwa vifo ambavyo vinatokea asilimia 70%
Aidha Dk, Husna alifahamisha kuwa kila mwaka watu milioni 15 wenye umri wa miaka 30 – 69 hufariki dunia kutokana na maradhi yasioambukiza.
“Mbali na hayo maradhi ya moyo, mshipa wa damu ndio maradhi yanayoongoza kuua watu ambapo Kwa mwaka mmoja watu milioni 17.7 huku magonjwa ya saratani watu milioni 8 hufariki dunia,maradhi ya njia ya hewa (magonjwa ya pumu) watu milioni 3.9 hufariki na maradhi ya kisukari watu milioni 1.6 hufariki dunia kila mwaka,” alifahamisha Dk, Husna.
Dk,Husna alieleza kuwa ripoti ya Wizara ya afya ya Zanzibar ya mwaka 2021 imeionesha kuwa asilimia 4.7% ya wagonjwa wanaolazwa hospitali ni kutokana na kisukari huku vifo vikiwa ni asilimia 9.5%.
“Kwa upande wa Zanzibar utafiti uliofanywa mwaka 2011 umebaini kuwa wanaofikia asilimia 33% wanaishi na shindikizo la damu, asilimia 3% kisukari, asilimia 18% hawafanyi mazoezi huku asilimia 2% ndio wanaotumia matunda,” alifahamisha Dk, Husna.
Akitoa maelezo ya kitendo hicho, Meneja wa maradhi yasioambukiza Zanzibar Dk,Omar Mohammed Suleiman alieleza kuwa maradhi yasioambukiza yamekuwa yakichukuwa nafasi kubwa katika kuiathiri maisha ya watu pamoja na kuleta ulemavu Kwa wanajamii.
Aidha Dk Omar alieleza kuwa magonjwa haya ambayo yasioambukiza hakuna mwanaadamu hata mmoja ambae anaweza kuyaepuka Kwa njia yeyote ile.
“Kwa upande wa maradhi haya hakuna hata mmoja wetu ambae ataweza kuyakwepa, wapo ambao Wana ugonjwa wa pumu, presha na hata kisukari na wote Hawa tunaishi nao katika familia zetu,” alifahamisha Dk, Omar.
Katika mafunzo hayo,waandishi wa vyombo mbalimbali Kisiwani Pemba walihudhuria ambapo mada kuu 4 ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na hali halisi ya maradhi yasioambukiza na vichocheo vyake, ugonjwa wa shinikizo la juu la damu na athari zake,ufahamu ugonjwa wa kisukari na athari zake pamoja na saratani.
MWISHO