Friday, January 31

VIDEO: UNDP KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA KUISAIDIA JAMII JUU YA DHANA YA UTAWALA BORA .

NA KHADIJA KOMBO – PEMBA.

Afisa  Mdhamini Ofisi ya Rais katiba sheria  Utumishi wa umma na Utawala bora Halima Khamis Ali Amezitaka jumuiya zisizo za Kiserikali  kuendelea kutoa mashirikiano katika   kuelimisha jamii  juu ya haki za binaadamu na misingi ya utawala bora ili kuendeleza   mshikamano  na Amani iliopo nchini  .

Akizungumza na wanaasasi za kiraia Kisiwani Pemba wakati akifungua mafunzo  juu ya haki za binaadamu na Utawala Bora  huko katika ukumbi wa Kiwanda cha makonyo Pemba amesema utawala bora ndio kila kitu katika nchi kwani kukosekana kwake  huashiria ufunjivu wa amani na kurudisha nyuma juhudi za maendeleo.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa uwezeshaji wa sheria na upatikanaji wa haki kutoka shirika la kimataifa la  UNDP kanda ya Zanzibar  Gramalied  amesema kutokana na umuhimu wa wanaasasi katika kuifikia jamii wameona iko haja ya kushirikiana na asasi hizo ili kuisaidia jamii juu ya kufahamu dhana ya utawala bora kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.

Naye  Katibu  wa Jumuiya ya Muungano wa asazi za kiraia  Pemba  (PACSO)   Sifuni Ali Haji amesema  kwa kushirikiana na asasi za kiraira  PACSO  itahakikisha elimu hio wanaifikisha kwa jamii ili  dhana hio iweze kutekelezwa kwa vitendo.

Mafunzo hayo ya siku nne yamewashirikisha   wanaasasi mbali mbali za kiraira kutoka Wilaya zote Kisiwani Pemba.

KUANGALIA VIDEO HII BOFYA HAPA