Wednesday, January 1

KOMBE LA NGO’MBE LAZINDULIWA RASMI.

NA SAIDI ABRAHMAN.

JUMLA ya vilabu 18 kutoka maeneo tafuati ya Wilaya ya Chake Chake, vimeanza mbio za kuwania kombe la Ngo’mbe michezo inayopigwa katika uwanja wa Ndugukitu.

Ligi hiyo iliyogawika makundi mawili ambapo kundi A likiwa na timu Boda boda, Salu Poo, Watanga, Big Night,Mti Pesa, Cossovo, Michakaeni, New Fletin na Tibirinzi.

Kwa upande wa kundi B, ni timu ya Mitumba, Kinje Boy, Machilii, Vikunguni Combine, NMB, Mkoroshoni, Vijana Machomanne, Small Sansiro na Ditiya.

Katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu ya Big Night na Cossovo, ambapo timu ya Cossovo iliibuka na ushindi wa bao 1-0, huku Mkoroshoni na Machalii wakatoka bao 2-2.

Mapema akifungua mashindano hayo Mwenyekiti wa Vijana CCM Mkoa Kusini Pemba Amina Abeid Mussa, alisema michezo sio ugomvi, bali hudumisha Umoja na Mshikamano.

Alisema michezo ni afya na upando miongoni mwa wachezaji, hivyo alitaka vijana kuendelea kudumisha amani na utulivu kupitia michezo.

Mapema msimamizi wa mashindano hayo Mohamed Rashid, alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya wachezaji, ili kuhamaisha soka la Zanzibar.

“Tanzania wanatumia ndondo, Unguja wanatumia yamle yamle na sisi Pemba tunakombe la Ngombe, itafika wakati tuwe na jina moja katika mashindano hayo na kuweza kutambulika,”alisema.

Nae Kassim Juma Mussa alisema Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Ngo’mbe, Mshindi wa Pili Mbuzi, watatu na wanne watapatiwa, pamoja na zawadi mbali mbali zitatolewa.

MWISHO