Saturday, December 28

HABARI PICHA:MAKAMU MWENYEKITI ASHIRIKI UJENZI WAMIRADI PEMBA.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiangalia ramani ya jengo la kitega uchumi la Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya CCM Mkoa huo.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiwa na tabasamu pamoja na baadhi ya Viongozi wa CCM Taifa na Mkoa wa Kaskazini Pemba, mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya Ngombe, kutoka kwa wanaCCM wa Mkoa huo, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya CCM Mkoa huo.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akipeana mikono kuashiria kupokea zawadi ya susu la Kuku na Mikungu ya Ndizi kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Marco Mbanga, ikiwa ni zawadi kutoka kwa wanaCCM wa Mkoa huo, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya CCM Mkoa huo.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiweka Tufali kuashiria kushiriki ujenzi wa eneo la chama cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni, litakalojengwa maduka ya biashara wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya CCM Mkoa huo
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiweka Udongo kuashiria kushiriki ujenzi wa eneo la chama cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni, litakalojengwa maduka ya biashara wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya CCM Mkoa huo
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mohamed Said Dimwa, akiwa amekamata konobao kuweka sawa udogo, akiashiria kushiriki ujenzi wa eneo la chama cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni, litakalojengwa maduka ya biashara wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya CCM Mkoa huo

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)