NA KHADIJA KOMBO -PEMBA
Wanawake nchini wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya usafi wa miili yao wakati wanapo pata hedhi ili kuepuka matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza.
Wito huo umetolewa na Dr. Rahila Salim Omar wakati alipokuwa akiwasilisha mada juu ya hedhi salama katika mafunzo ya waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali viliopo Kisiwani Pemba.
Amesema kuna matatizo mengi ya kiafya ambayo wanawake wanaweza kuyapata iwapo hawatochukua tahari wakati wanapo pata hedhi ikiwa ni Pamoja na tatizo kubwa la kupata kansa ya shingo ya kizazi.
Pia amewataka akina mama hao kuhakikisha wanapo kuwa katika hali hiyo wanajisafisha angalau mara tatu kwa siku, kutumia nguo safi Pamoja na kuosha vizuri nguo hizo na kuzianika juani ili kuuwa vijidudu vinavyoweza kubakia katika nguo hizo.
Akizungumzia kuhusu tabia kwa baadhi ya akina mama kuweka vitu vya matukato sehemu za siri na kusema kuwa hairuhusi kuweka kitu chochote kwenye uke kwani ni moja kati ya sababu inayo sababisha kupata kansa ya shingo ya kizazi.
Amesema kwa Mujibu wa takwimu inaonesha karibu asilimia 90/ ya wanawake katika ukanda wa pwani wanaweka vitu sehemu za siri na kusababisha kupata maradhi tofauti ya mambukizo.
MWISHO