Sunday, November 24

VIDEO: WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUTENGA MUDA WA KUZUNGUMZA NA WATOTO WAO.

NA KHADIJA KOMBO- PEMBA.

Wazazi na walezi  nchini  wameshauriwa kutenga muda  wa  kuwa karibu na Watoto wao ili waweze  kuzungumza nao mambo mbali mbali yanayohusu makuzi yao.

Akifungua mjadala   juu ya kujadili changamoto zinazo wahusu Watoto kwa wazazi, walezi Pamoja na wadau wengine wa Watoto huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Chake Chake Mrajis wa asasi za kiraiya Pemba Ashrak Abdalla Ali amesema hivi sasa wazazi na walezi   wamekuwa wakijishughulisha na harakati zao za kujitafutia Maisha Zaidi na kukosa muda wa kukaa na Watoto wao na kujua matatizo yanayowakabili.

Kwa Upande wake Mongozaji wa mjadala huo Mratib Wa TAMWA Zanzibar kwa upande wa Pemba Fat-hiya Mussa Said amesema ni vyema wazazi na walezi   kuhakikisha muda wote wanakuwa karibu na Watoto wao ili waweze kuwa salama wakati wote.

Kwa upande wao washiriki wa Mjadala huo  wameshauri wazazi kuangalia namna ya kurudisha mfumo wa malezi ya pamoja ili kuwaweka watoto katika mazingira salama

Mjadala Huo ambao umewashikisha wanajamii, wanaharakati kutoka jumuiya tofauti zisizo za kiserikali, masheha  Pamoja na waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vilivyoko  Kisiwani Pemba umeandaliwa na  Umoja wa Jumuiya zisizo za Kiserikali Pemba ( PACSO) chini ya ufadhili wa Irish Aid.

MWISHO.

 

ANGALIA VIDEO HII KWA KUBOFYA HAPO CHINI