AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
Baadhi Wanafunzi wa kike wanatumia Matambara wakati wa Hedhi kutokana na kutoweza kumudu Bei Ya Taulo Baadhi ya Wanafunzi Huku wengine Tukiona kama ni Ugonjwa Ambao kwa Tamaduni zetu kumueleza Baba au mama Tunaisikia Aibu sana, kwa kweli, inaskitisha mno kwani Matambara hayo yanaweza kuacha Madoa ya hedhi kwenye nguo zetu za Skuli Pamoja na nguo za ndani”. Alidai Fatma Abdalla Mbarouk Kutoka skuli ya Sekondari Msuka.
” Wahisani Waliangalie na Suala la Maji katika skuli yetu ya Msuka Sekondari Wanafunzi wa kike Tunapitia changamoto Kipindi cha Hedhi, na naamini sio Skuli yetu peke na yengine pia” Ruwaida Salum Hamad Mwanafunzi Msuka Sekondari Wilaya ya Micheweni.
Ofisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Muhammed Nassor Salum amesema kuwa licha ya jitihada za Serikali na wadau bado tatizo la Hedhi Salama Skulini linahitaji Mikakati Endelevu, kutokana na Umuhimu wake .
“Wizara ya Elimu inafanya Jitihada mbalimbali ikiwemo kuimarisha Miundo mbinu kuwa Rafiki kwa watoto wakike, Kutumia vyumba maalum wanapokuwa katika Vipindi vya Hedhi, waalimu washauri , Taulo zinakuwepo Mashuleni Maji lakini bado inakuwa havijitoshelezi kwa vile suala hili ni endelevu kwaio Tunaendelea na namna bora ya kuliangalia suala hili katika mikakati endelevu Ili kuona watoto wakike hawakosi masomo wanapokuwa katika Mzunguko.
Ikumbukwe kuwa kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira kupitia Mpango Endelevu ya Maji na Usafi wa Mazingira Skuli na vijijini Mwaka 2020/21, ilieleza kuwa Serikali ya Tanzania imeweza kujenga Miundo mbinu ya vyoo vikiwemo vya Wanafunzi wenye ulemavu pamoja na sehemu ya Hedhi salama ambayo ina vifaa muhimu vinavyohitajika katika shule 835 kwenye Mikoa 17 pekee.
Aidha Kwa Mujibu wa Taarifa iliyitolewa na Ofisi ya Takwim Tanzania (NBS) juu ya masuala ya Maji na usafi Mazingira skulini mwaka 2018 inaonesha asilimia 66.8 ya shule ndizo zina huduma ya Hedhi salama ambapo kati ya hizo zilizobainika kuwa na viteketezi ni asilimia 24 huku asilimia 22.8 zinatupa taka kwenye mashimo na 19.5 zina vichomea Taka visivyokidhi.
Hata Hivyo kwa Visiwa vya Unguja na Pemba Serikali Ya Mapinduzi kupitia Wizara ya Afya Kitengo Cha Lishe Kilifanya Utafiti Mdogo Mwaka 2022 karika skuli mbali mbali Na kubaini kuwa Asilimia 25 ya Mahudhurio ya Skuli kwa Wasichana wakati Hedhi, hawahudhurii ioasavyo, huku Ikibainisha kuwa Asilimia 12.5 wakihudhuruia bila kuwa na Usomaji mzuri kutokana na sababu mbali mbali za Kiafya.
JEE UTI NI NINI?
Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na Makala hii walieleza hofu yao juu ya Kupata Maradhi ya UTI
UTI kwa Wanawake ni maambukizi ya Mfumo wa Mkojo kwa wanawake ambao huhusisha figo, kibofu cha mkojo Mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo pamoja na mrija unao unganisha figo na kibofu cha mkojo,Ambapo Mambukizi haya kwa kiasi kikubwa husababishwa na Bakteria Jamii ya Escherichia( E.coli), ambao moja kwa moja huathiri Mfumo wa Mkojo, Na Wanawake Huweza kupata Hatari ya Maambukizi haya endapo atakuwa katika hali zifuatazo, Kinga ya mwili kutokuwa imara, Kutumia vifaa au dawa za kuzuia mimba, Kupungua kwa homoni ya Estrogen, Ugonjwa wa kisukari, Kufanya ngono isiyo salama, Mimba, Pamoja na Kutumia choo kichafu.
Mwanamake huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuugua ugonjwa huu pamoja na kujirudia mara kwa mara kwa kuwa mrija wa mkojo huwa ni mfupi sana tofauti na mwanaume, pia tundu la uke huwa karibu na sehemu ya haja kubwa hivyo ni rahisi kwa Bakteria kutoka kwenye Choo kuingia ukeni jambo ambalo husababisha kuongezeka kwa Matumizi ya Vyoo mara kwa mara kutokana na Kupatwa na maumivu wakati wa haja ndogo, Kujisaidia haja ndogo mara kwa mara isiyotoa mkojo mwingi, Kujisaidia mkojo mweusi au ulio na chembechembe za damu na harufu kali, Maumivu ya nyonga, Uchovu, Homa na kutapika, Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo.
Alphonce Mbarambe Gura ni Mwanasheria kutoka Taasisi ya Legal Service Facility Zanzibar alisema kuwa Suala La Hedhi linatambulikana kikatiba kama ni haki ya Msingi kati ya Haki za Binaadamu kwa vile suala hilo linagusa moja kwa moja Utu.
“Lazima suala la Hedhi Salama liangaliwe kwa upana wake hivyo ni lazima Watoto wakike wenyewe waweze kujua ni jinsi gani suala la hedhi Salama ni muhimu kwao, haki ya kupata vifaa vya kujisitiri kwa gharama nafuu ambavyo ni salama , kupata Mazingira wezeshi Skuli na Nyumbani ya kubadilishia nguo Maji ya Salam kwa vyovyote hivi wanayo haki ya kudai endapo watakuwa Skuli ama Majumbani ni haki inayitambulika kisheria Hedhi ni Haki ya Utu, Utu unatakiwa kuthaminiwa wito wangu wanafunzi waamke kusoma kujua haki zao na waweze kuzidai kisheria”.
Mwache Juma Abdalla ni Mwalimu Mkuu skuli ya Conecting continent Sekondari anasema Wanafunzi waliowengi Hukosa Furaha na hamu ya kusoma Wanapokuwa katika kipindi Cha Hedhi kutokana na Sababu mbali mbali jambo ambalo uongozi wa Skuli hiyo kutumia Umakini Mkubwa ikiwemo masomo ya Muda wa ziada, katika Kufundisha ili kuepusha ufaulu mbovu kwa Wanafunzi wa kike.
Mtumwa Said Khamis Ni Mwalimu Mshauri na nidhamu Skuli ya Madungu Sekondari anasema “Mara chache sana na Wanafunzi ndio hunifuata Kueleza Changamoto wanapopatwa na dharura hiyo, Tunatumia uzoefu wetu kugundua hizo changamoto na kuwasaidia hawasemi.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar Kupitia Mradi wa Afya ya Uzazi wamesema Changamoto Zinazokabili Wanafunzi juu ya Masuala ya Hedhi Salama kwa Wanafunzi wamesema Wanazipatia Ufumbuzi kwa Kuandaa Elimu maalum kwa Waandishi wa Vyombo mbali mbali na kueleza Athari ili Jamii na wahisani mbali mbali waweze kuzibaini na kuzipatia Msaada wa Haraka.
Kama ambavyo Taasisi mbali mbali zimekuwa zikiendelea kutoa msaada wa Taulo za kike kwa baadhi ya wanafunzi kadhalika Serikali na Wadau iliangalie suala hili la Elimu, Maji, Vyoo vya Matundu, pamoja Na Majaa (Dampo) , Uoatikanaji wa Taulo za kike kwa wote kwa garama nafuu, ili kuimarisha Zaidi Afya ya Hedhi salama Kwa wanafunzi wa Kike kwa vitendo .
Mwisho.