

NA MWANDISHI WETU.
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeendelea na jitihada za kutokomeza changamoto ya Tembo wanaovamia makazi na mashamba ya wananchi katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi ambapo wamekuja na mbinu ya kutengeneza tofali lilichomwa lenye mchanganyiko wa kinyesi cha mnyama pamoja na pilipili.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya namna ya kukabiliana na Tembo kijijini Mkoka Ruponda wilaya ya Nachingwea, Afisa Mhifadhi Mkuu Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania Kanda ya Kusini Mashariki, Linus Ezekiel Chuwa alisema kuwa mbinu ya kuchoma tofali lililotengenezwa na kwa kinyesi cha mnyama pamoja na pilipili kutasiadia kuwafukuza Tembo Kwa kuwa mnyama huyo hapendi harufu ya pilipili.
Chuwa alisema kuwa serikali imekuwa ikutumia mikakati ya muda mrefu katika kukabiliana na Tembo, TAWA kwa kushirikiaha na PAMC Foundation imetoa mafunzo ya namna yakukabiliana na wanyama hao kwa kwa kuweka uzio wenye mchanganyiko wa pilipili na mafuta machafu pamoja na matumizi ya ndege Nyuki, matumizi ya gari Maalum na tofali la pilipili.
Alisema kuwa kuwafundisha mbinu hizo zitasaidia wananchi kuwafukuza Tembo na kuepukana na madhara ambayo yamekuwa yanatokana na mnyama huyo.