Thursday, January 16

Vijana washauriwa kujiunga na vikundi vya ushirika ili kujipatia kipato.

NA FATMA HAMAD PEMBA,

Vijana wameonywa  kuepuka kukaa katika vigenge viovu ,na badala yake wajiunge  na vikundi  vya ushirika,  ili waweze kujipatia kipato cha halali.

Ushauri huo umetolewa na katibu wa kikundi cha ushirika  mapambano cooperative kinacho jishuhulisha na ufugaji wa Samaki, kaa, kamba  na mboga mboga  Bishara Muhammed Mussa mbele ya  wanakikundi hao,  mara baada ya kutembelewa na wajumbe kutoka wizara ya uchumi wa Buluu na shirika la IUCN kutoka Tanzania bara huko Sizini wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazi Pemba.

Alisema wakati umefika  kwa vijana  kuwamka na kujiajiri wenyewe, na sio kukaa tu vigengeni na kusubiri ajira Serikalini.

‘’Vijana  mtakapo jiajiri mtaepukana na  vitendo vya wizi, ubakaji na ujambazi,’’ alishauri katibu.

Aidha  alieleza kuwa  sera ya Serikali  ya mapinduzi ya Zanzibar ya uchumi wa buluu  unaelekeza zaidi kwenye bahari, hivvyo  aliwasisitiza  viajana hao   kukiendeleza kikundi chao kwa juhudi zote, jambo ambalo litawawezesha kupata ursa mbali mbali za kimaendeleo.

Mapema mwanakikundi Khadija  Ali  Juma alieleza kuwa ameamua kujiunga kwenye kikundi  cha ujasiriamali, ili aweze kujipatia kipato  kitakacho msaidia katika familia yake.

Aidha alisema mafanikio hayaji tu kama ndoto, hivyo ni vyema kuwa wavumilivu kupitia changamoto zinazowatokezea ili waweze kukiikisha mbele kikundi chao.

Akieleza  changamoto zinazowakwaza  kikundini  hapo  amesema ni vitendea kazi, ikiwemo mabero  pamoja  mapauro.

Mwenyye kiti wa kikundi hicho Khalfan Hamad Khalfan alieleza kuwa  matarajio yao ni kuhakikisha wamekuwa wazalishaji wakubwa  wa mazao ya baharini.

‘’Tunatarajia kuzalisha  Tani moja  ya kaa, na  Tani moja ya Kamba  kila baada ya miezi miwili, na tani moja ya Samaki ndani ya kipindi cha mwaka mmoja,’’ alisema mwenyekiti.

Hivyo aliomba wizara ya uchumi wa buluu kujitokeza na kuwaunga mkono vikundi ambavyo vimewekeza juhudi zao kwenye maeneo ya bahari, ili waweze kunufaika na fursa zilizomo,  ndani ya  sera ya uchumi wa bluu.

 Nae  Afisa kutoka wizaa ya uchumi wa buluu Pemba Mohd Ali  pamoja na wajumbe kutoka  shirika la International  Union for conservation of Nature  [IUCN] walifika katika kikundi hicho na  kuangalia maendeleo yao, na kuelewa changamoto zinazo wakabili  wanakikundi hao  na kuweza kutatuliwa.

Kkikundi hicho ambacho kinawanachama 17 wanaume 8, na wanawake 9, kilianzishwa  rasmi mwaka 2013.