Wednesday, January 15

Walimu wa sanaa kufuata mila, silka na utamduni wa kizanzibari.

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, akiwasikiliza wanafunzi wa skuli ya Madungu Msingi, wakati wakiwasilisha ngonjera zao, kuelekea kilele cha tamasha la elimu bila ya malipo hafla iliyofanyika chuo cha amali VitongojiWilaya ya Chake Chake.

 

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, amewataka walimu wanaosimamia na kufundisha sanaa za utunzi Pemba, kufuata maadili, sikla na Utamaduni wa mzanzibari katika kuwafundisha wanafunzi sanaa mbali mbali maskulini.

Alisema wanafunzi wengi wanaoshiriki katika sanaa ikiwemo Ngojera, tenzi, mashairi na michezo wamekua wakiiga mahadhi ya kigeni au wasanii waliopita, jambo ambalo halitowajenga katika sanaa iliyobora.

Katibu mkuu Fatma aliyaeleza hayo mara baada ya kusikiliza na kuona sanaa mbali mbali zilizowasilishwa na wanafunzi wa Mikoa miwili ya Pemba, ikiwa ni kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya elimu bila ya malipo mwaka huu.

Alisema sana ni mmoja kati ya masomo yanahitajika kuendelezwa katika jami, hivyo walimu ni vyema kuwanda wanafuzi katika madili mazuri, wakati wa kuwasilisha sana zao ili kuendeleza utamaduni uliyopo visiwani zanzibari.

“Watoto ni watoto ili kuzionesha sanaa za Pemba, kuwa nzuri na kufanya vyema katika mashindano ya elimu bila ya malipo, vizuri tukatafuta mahadhi mazuri ambayo yataweza kuibua hisia kwa jamii pale watakaposikiliza,”alisema.

Aidha alihimiza suala zima la umoja mshikamano, kwa walimu ili kuifanya sanaa kuendelea kuwa bora kwa jamii, zaidi pale watoto wanapokosea kutokusita kuwarekebisha.

Akizungumzia suala la ujenzi wa uwanja wa michezo mchanganyiko, alisema Pujini ni moja ya maeneo ambayo yanakusudiwa kujenga viwanja mbali mbali vya michezo yote ili kuwapa nafasi wanafunzi kuonyesha sanaa zao.

Kwa upande wake Afisa mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Pemba Mohamed Nassor Salim, aliyomba wizara ya habari kulitumia eneo la skuli ya elimu mjumwisho pujini kujenga viwanja vya michezo ya sana, kwani wataweza kuvikuza vipaji vya vijana vilivyopo kisiwani Pemba.

“Vijana wangu nawaombeni mara hii tamasha linafanyika Pemba, vikombe vinatoka Unguja kuja Pemba nawaombeni musije mukaniangusha nataka vikombe vyote vibaki Pemba,”alisema.

Nae afisa mdhamini wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Pemba Mfamau Lali mfamau, ameitaka wizara ya elimu kuendeleza mashirikiano ya pamoja na wizara ya habari, katika michezo ili kukuza na kuviendeleza vipaji vya wananfuzi viweze kuwasaidia hata baada ya kumaliza masomo yao.

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, akiwaongoza majaji wakati wakusikilisha sanaa mbali mbali ngojera, ushairi, ngoma, maigizo kuelekea kilele cha tamasha la elimu bila ya malipo hafla iliyofanyika chuo cha amali VitongojiWilaya ya Chake Chake.

Akitoa neno la shukura afisa elimu mkoa wa kusini Pemba Mohammed Shamte, alisema iwapo wanafunzi wataandaliwa vizuri katika michezo, huongeza ufaulu mzuri kwenye masomo yao hivyo ni vyema kwa walimu na wazazi kutumia muda nzuri wa kuwafundisha masomo yao na sana.

 

Katika mandalizi hao ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya elimu bila malipo Zanzibar, sana mbali mbali zimewasilishwa zikiwemo ngojera, ushairi, ngoma, maigizo huku kilele chake kikitarajiwa kufanyika kisiwani Pemba Septemba 23 mwaka huu.

 

MWISHO