RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameinasihi jamii kuongeza upendo na ushirikiano hasa kwenye makundi maalum na kuwasaidi kwa kila hali.
Al hajj Dk. Mwinyi, alitoa nasaha hizo kwenye Msikiti wa Ijumaa Miti Ulaya, Mkoa wa Mjini Magharibi, alikojumuika na waumini wa dini ya Kiislamu kwa ibada ya sala ya Ijumaa.
Rais, Al hajj Dk. Mwinyi, amesema jamii inawajibu wa kuyahurumia makundi hayo wakiwemo watoto hususani yatima, wazee, watu wenyeulemavu na wanawake wajane.
Alisema, Waislam wanawajibu wa kuwa karibu na jamii zao kwa kuonesha upendo hasa kwenye makundi hayo, Al hajj Dk. Mwinyi aliwaeleza waumini hao mwamba misikiti pia ina wajibu wa kujadili jinsi ya kuyasaidia kwa wema makundi hayo.
“Ndani ya jamii zetu, tunapaswa kuwahurumia zaidi makundi maalumu, wakiwemo watoto yatima ambao bado hatujaweza kuwalea vizuri”
Aidha, Al hajj Rais Mwinyi aliitaka jamii kuendelea kuhimizana juu ya malezi bora kwa watoto hao, kuwazidishia upendo, kuwajali na kuwatunza vizuri.
Akizungumzia kundi la wanawake wajan
e, Al hajj Dk. Mwinyi aliwataka viongozi wa misikiti kuona umihimu wa kujadili jinsi ya kuwasaidia kwa wema wajane, watu wenye ulemavu na wazee ili kujenga jamii yenye umoja, upendo na mshikamano.
Naye, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume aliisisitiza jamii juu ya kuwahurumia wazazi wawili pamoja na wazee wasiojiweza kwa kuongeza upendo kwao na du’a njema kwa Mwenyezi Mungu awahurumie kama alivyowahurumia wao walipokuwa wadogo.
Mara baada ya sala ya Ijuma, Rais Al hajj Dk. Mwinyi alihudhuria Maziko yaí Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini, Marehemu Mgana Zidi Khamis aliyefariki dunia asubuhi na kuzikwa kijini kwao kwa Paje.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR