Thursday, January 9

Wakulima wa mboga mboga na matunda kisiwani Pemba wametakiwa kuchunguza afya ya Udongo kabla ya kulima kuepuka hasara.

Na Amina Ahmed-Pemba.
ZAIDI ya wakulima 120  wa mboga mboga na matunda   kutoka maeneo mbali mbali ya  kisiwa cha Pemba  wamepatiwa mafunzo maalumu   juu ya afya bora ya udongo  na usimamizi wa rutuba kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo Zanzibar.
 Akitoa elimu  elekezi  katika mafunzo hayo mkuu wa division ya utafiti wa udongo na mimea  Zanzibar Ali Hamad Ali alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni  kuwasaidia  wakulima kuweza kuchunguza  afya ya udongo kabla ya kulima mazao yao  kuepuka hasara na kujipatia faida kupitia kilimo chao.
 “Udongo ndio tegemeo kubwa la wakulima katika masuala ya kilimo tumeona ni vyema kufikisha elimu hii kwa wakulima   kutokana na waliowengi kukosa elimu hii na kupata hasara mbali mbali ikiwemo mazao kuharibika pamoja na miche” .
Alisema  kutokana na wakulima wengi kuendelea kutumia mashamba ambayo yalishatumika  kwa muda mrefu na  mashamba hayo kuondokana na virutubisho na kupelekea kutofikiwa malengo ya kunufaika na mazao kwa wakulima  taasisi hiyo imeamua kuwa karibu na wakulima kutoa elimu hiyo itakayobadilisha maisha yao  .
“Ili kufanya kilimo kiwe endelevu na wakulima waweze kupata tija na mazao mazuri  tumeona ni bora kueneza elimu hii ya uhuwishaji  na utunzaji wa udongo lengo ni kulima kitaalamu kwa kutumia teknolojia yenye kuutambua udongo”.
 
 AkitoaeElimu  elekezi kwa wakulima hao Asha Muhamed  Shoka  kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar kitengo cha udongo amewataka wakulima hao kufanya uchungizi  na kupima udongo kabla ya kuanza harakati za kilimo ili kuwasaidia kutambua aina za udogo.
“Kupima udongo kutaweza kuwasaidia wakulima kujua aina gani ya udongo inafaa kwa kilimo au mazao fulani hiyo itawadaia kuwaepushia hasara  mbali mbali mnazozipata katika mashamba yenu”.
Katika udongo kuna P, H tofauti tofauti  ambazo  ni maalum kwajili ya mboga mboga za aina fulani  kuupima kabla ya kuanza kulima ni bora zaidi  ili kuendana sambamba na teknolojia katika kukuza kilimo.

Wakizungumza mara baada ya mafunzo hayo baadhi ya wakulima  waliopatiwa mafunzo  Maryam Rashid salum  Ali kutoka Mjini Ole  pamoja na  Mafunda Bakari Ali wamesema  elimu hiyo itasaidia kulima kilimo cha kisasa ambacho  kitawasaidia kuikomboa kiuchumi ambapo pia wamesema wataifikisha kwa wakulima wengine ambao walikosa mafunzo hayo ili iweze kuwanufaisha.
Mradi wa kufikisha  Teknolojiya ya  kutunza afya  ya   udongo kwa wakulima wa mboga mboga, na matunda World Vegetable  umefadhiliwa na  washirika wa maendeleo  mbali mbali  ya maendeleo ikiwemo  IFDC pamoja na USAID  ambapo wakulima, mabwana shamba,  viongozi ,wanshehia na maafisa kilimo wilaya zote nne za Pemba walishiriki katika mafunzo hayo  Ambapo Mafunzo hayo ya siku moja  yalifunguliwa  na Afisa Mdhamini wizara ya kilimo Pemba .