NA ABDI SULEIMAN,PEMBA
NAIBU Katibu Mtendeji Idara ya Program Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Abouud Idd Khamis, amesema maafisa Habari, maafisa Uhusiano na waandishi wa habari wanapaswa kutoa taarifa za uwazi kwa wananchi, ili kuendana na teknolojia za kisasa katika upatikanaji wa habari.
Akizungumza kwenye mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwashirikisha maafisa habari, maafisa uhusiano na waandishi wa habari, kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar na kufanbyika mjini Chake Chake.
Alisema mafunzo hayo yanalenga kuimarisha uwezo wa maafisa habari na maafisa mawasiliano, maafisa uhusiano wa Umma na waandishi wa habari, wafanyakazi wa vyombo vya habari mbali mbali kutoka taasisi za serikali na binafsi, katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na taasisi zao kwa wananchi.
“Ukweli usiopingika maafisa hawa wanamchango mkubwa katika kuelimisha jamii kuhusiana na masuala mbali mbali, yanayohusu taasisi wanazozifanyia kazi, pamoja na kuuamsha ari na ushiriki wa wanachi kwenye maendeleo ya taifa,”alisema.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, alisema ni muhimu na kwa wanahabari kuwa na uwelewa wa kutosha, juu ya teknolojia ya mawasiliano na vyombo vya habari vya kisasa, ili kuelewa jinsi mitandao ya kijamii, program za simu na majukwaa mengine ya kijiditali yanavyofanya kazi.
Akizungumza kwa niaba yake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Hassan Khatiba Hassan, alisema kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani, jamii imekua na wigo mpana wa kupata taarifa nyingi na kwa haraka, hivyo ni muhimu kuwa wabunifu katika mawasiliano, ili maudhui yao yaweze kueleweka kwa urahisi na kuwavutia watu wanaowalenga.
“Kuwashirikisha maafisa habari na maafisa uhusiano na waandishi wa habari, ni mjumuiko muhimu sana wa kufanikisha kazi kwa pande hizo husika, zinapaswa kujenga uhusiano mzuri wa kikazi kwa vyombo vya habari na wadau wa umma kwa jumla,”alisema.
Hata hivyo aliwataka maafisa habari kuwa makini na kuhakikisha wanataoa habari sahihi za kuaminika, kuwa na mkakati malumu wa kukabiliana au kushuhulikia changamoto zinazojitokeza katika taasisi wanazozifanyia kazi.
”Lazima muwe mstari wa mbele pale panapotekea taasisi kusemwa vibaya, kutoa maelezo ya haraka inapotokea kwa ajili ya taasisi husika,”alisema.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo yaho kutoka chuo cha Taifa Zanzibar (SUZA) Imane Duwe, alisema uwepo wa maafisa habari ni watu muhimu wa taasisi, hivyo lazima kuhakikisha wanakua karibu na vyiombo vya habari.
“Unapokua karibu na vyombo vya habari unahakikisha kazi zao zinafanyika kwa umakini na haraka kwa kuhabarisha umma na kujua kilichofanyika.
Hata hivyo aliwataka waandishi hao kuangalia mipaka ya utoaji wa taarifa zao, sambamba na kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Akichangia katika mkutano huo, Afisa habari kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Heri Juma Basha, alisema bado watu wa IT katika ofisi wanajifanya ni waandishi wa habari, hali inayopelekea kuwepo kwa watu wa habari wasio na vyeti.
Mwandishi wa ITV Pemba Suleiman Rashid Omar, alisema mafunzo hayo ni muhimu na yataweza kuleta mabadiliko katika taasisi wanazozifanyika kazi.
MWISHO
Abdi Juma Suleiman