Friday, December 27

NGWARE ni michezo wa asili ndani ya Wilaya ya Micheweni

WACHEZAJI wa Mchezo wa Ngware wakioneshana uhodari wao wakucheza mchezo huo katika moja ya sherehe za Vijan Kisiwani Pemba

 

NGWARE ni michezo wa asili ndani ya Wilaya ya Micheweni

  • Wachezaji hujiandaa kwa kunywa mtindi
  • Tayari umeshajizoelea mashabiki wengi ndani ya wilaya hiyo

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

NGWARE ni Kupinga mtu mtama naweza kusema hivyo kwa upande mmoja, upande wa pilia ni mchezo unaotumia miguu na mikono katika uchezaji wake.

Hili neno Ngware ni neono Fulani, mchezo huu unaweza kusema hauna tafauti na mieleka kutokana na uchezaji, ukamataji wake, hata kuangashuna kwakwe na kupatikana kwa mshindi.

Katika kisiwa cha Pemba Wilaya ya Micheweni, ndio mchezo huo unakochezwa kwa sasa tokea miaka 30 iliyopita, kwa afrika ni mkubwa sana na zaidi Senegali unachezwa, duniani ni Japani na hutumika wachezaji wanene (Wrestiling).

Kwa sasa mchezo wa ngware haumo tena kwenye mashindano ya Olympic, mara ya mwisho mchezo huo ulitolewa mwaka 2020, kiwanja chake kinatakiwa kijengewe juu kidogo kama cha boxing, ili kuwafanya watu weweze kuona pande nne zote ziwe na futi 20.

Katika wilaya ya micheweni baada ya kuona vijana asili na urithi wao umeanza kupotea, wamelazimika kuufufua mchezo huo na sasa umerudi kwa kasi kubwa, kama ilivyokuwa kwa wazazi wao waliopita

MCHEZO WA NGWARE UNACHEZWA VPI

Omar Khatib Kombo anasema lazime kuwe na timu mbili A-B, kila timu inatoa mchezaji mmoja, ambapo watakua katikati na mwamuzi mmoja wa kuamua mshindi wa mchezo huo.

Anasema wachezaji hukamatana mikono kwa ukakamavu wa hali ya juu, hapo tena ndio wanapopigana Ngware (mtama) ili mmoja wapo amuwangushe mwenzake chini na kuwa mshindi.

“Unapotaka kucheza lazima uwe na nguvu, kwani mchezo huo unaotumia nguvu zaidi ili mshindi apatikane kwa kumuangushwa mwenzake chini.

WANAMICHEZO WANASEMAJE WAO

Khamis Ali Haji mkaazi wa shehia ya Majenzi Wilaya ya Micheweni, anasema sababu iliyopelekea kuingia katika mchezo huo ni kuupenda tokea utotoni mwake.

“Mimi nilimuona baba yangu akicheza na kunichukua kila mara, ghafla nilijikuta nacheza na mimi tena mpaka sasa nimo katika mchezo huu,”alisema.

Anasema tokea hapo amekua mchezaji mkubwa wa mchezo huo, hali iliyopelekea kuwahamasisha wenzake kushiriki kikamilifu, kucheza na sasa Wilaya nzima Micheweni imekua na timu hizo.

Aidha anasema licha ya kutumia kipindi cha Ramadhani usiku kucheza, lakini kwenye mashidano na sherehe za skukuu wanacheza jioni na mchana.

“Kwetu ni jadi mchezo huu kucheza, vijiji ambavyo vinacheza ni shumba mjini, kwale, mjini wingi, maziwa ngombe, kiuyu, micheweni mjini na chamboni, ndio waasisi wa mchezo huu walikotoka,”amesema.

Nae Salim Hamad Khamis Mkaazi wa Shumba Mjini, anasema sababu ya kuurudisha mchezo huo ni kuwafanya vijana kuepukana na vikundi viovu, kukaa maskani bila ya kutokua na chakufanya.

Amesema kwa sasa vijana wanaenda na wakati, michezo na ngoma nyingi zipo ndio wakaamua kuufufua mchezo huu, ili kuthamini juhudi zilizofanywa na wazee wao katika kuulinda utamaduni huo.

Salim amewataka vijana kujiunga katika mchezo huo, ili kuachana na tabia ya kukaa vijiweni bila ya kua na kazi maalumu, hali inayopoelekea kujiingiza katika vikundi viovu.

WAZEE WANASEMAJE JUU YA MCHEZO HUO

Mzee Kombo Mbwana Haji (60), anasema ufahamu wake mchezo huo ameukuta, ukichezwa jioni baada ya wazazi kurudi shamba kuvuna mtama au uwele.

Anasema mchezo huo ni mashuhuri katika wilaya nzima ya Micheweni, umeanza kuvuta hisia za watazamaji wengi na vijana sasa kucheza kwa ushindani.

“Kipindi hicho wazee wakicheza kama burudani ya kawaida, mimi mwaka 1972 hadi 1973 nakumbuka kutoka kwa wazee, baada ya kushiba maziwa yao mabivu kwa muda ya miezi miwili ndani ya kitungu, hapo ukiwaona wanagotana kiufupi mpige mpige mpaka wanaangushana,”amesema.

Akizungumzia sababu ya vijana kucheza Ramadhani usiku, anasema mchezo huo ni asili wao wakicheza jioni, vijana wameamua kuurudisha urithi wao ila wanalazimika kucheza usiku baada ya kushiba, kwani bado hamasha ya mchezo huo upo kwa watu wote.

Anasema tayari vijana wengi wameanza kuupenda, kwani upo kama ngao au zaidi kujilinda, kwa vile Unguja na Tanzania bara iko michezo ya mieleka au karati

Nae Haji Khamis Omar (56) mkaazi wa kwale Micheweni, anasema wazee kwao ilikua kama kupongezana baada ya kumaliza kuvuna uwele na mtama, lazima wacheze mchezo huo baada ya kazi kubwa walioifanya kwenye kilimo hicho.

Anasema zaidi wazee walikuwa wanacheza jioni, tena baada ya kumnywa mtindi kwa muda wamiezi miwili, ikiashiria kutia nguvu mwilini, hapo huoneshana umwamba wao kwa kucheza ngware.

Haji anasema hivi sasa vijana wamefanya jambo kubwa na lakuthaminiwa, baada ya kuufufua mchezo huo ambao ulionekana kuanza kupotea kwa kukosa wachezaji wenye nguvu.

“Wachezaji wanaocheza lazima wawe na nguvu, kwa sasa vijana wameanzisha timu za mitaa kwa kucheza mchezo huu, tayari umeshaanza kujizoelea mashabiki, kutokana na ushindani wa kupigana ngware,”amesema.

Aidha amewapongeza vijana kwa ujasiri na uwezo wao wa kurudisha mchezo huo, waliokua wakiucheza ikiwa ni utamaduni na asili kwa wananchi wa micheweni.

VITUNGU ambavyo walikuwa wakitumia wazee katika kutilia mtindi (maziwa mabivu), wakati wakijiandaa na mchezo wa ngware baada ya kumaliza mavuno ya uwele na mtama.

MSIMAMIZI WA MCHEZO HUO ANASEMAJE

Rashid Khamis Othaman mkaazi wa kwale Michweni, anasema mchezo wa ngware ulikua ukichezwa baada ya mavuno ya uwele na mtama, ili wachezaji kuonesha uhodari wao katika kilimo na kufuatia kupata mavuno mazuri angalau gunia saba hadi 10.

“Hapa Micheweni kipindi hicho, mchezo huu ulikuwa unachezwa katika vijiji viwili, maziwa Ngombe na kijiji cha Wingwi Maavi, sasa vijiji vyote vinachezwa mchezo huu baada ya kuufufua upya na kuhamasisha vijana,”anasema.

Anasema zaidi wazee walikuwa wakicheza kama tamaduni na kupongezeza, baada ya mavuno kutokana na ushindani waliokuwa nao kwenye kilimo hicho.

Rashid anasema walikua wanatumia Vitungu kunywa maziwa mabivu (mtindi) kupata nguvu, pamoja na kuvaa nguo maalumu kwa ajili ya uchezaji ili zisiwaletee matatizo wakati wa mchezo huo unapoendelea.

Amefahamisha kwamba mchezo huo ulikuwa ukichezwa na rika tatu, moja wazee, vijana na watoto wenye umri wa miaka 8 hadi 10, zaidi wakijengwa kujilinda na ukakamavu, huku wachezaji wanapaswa kuwa watano hadi 20, waliobakia hushiriki upigaji wa kofi.

USHIRIKI WA WANAWAKE UKOJE

Rashid Khamis Othaman anasema bado hawajaweza kushiriki mchezo huo, kutokana mchezo huo kutumia nguvu zaidi, pamoja na mila na tamaduni za kizanzibari zilivyo.

“Huwezi kumuona mwanamke huku kwetu anacheza mchozuu, kwanza mavazi gani atakayovaa pia kucheza mbele ya wanaume kwetu halikubaliki,”amesema.

Aidha amesema iwapo wakitokea wanawake kucheza basi yupo tayari kuwafundisha, pamoja na kuwapatia eneo maalumu kwa ajili yao ili kutokuchanganyika na wanaume.

IDARA YA UTAMADUNI PEMBA INAMTAZAMO GANI

Mratib idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Hamad Ali Haji, anasema idara unaufahamu mchezo huo na tayari wameshaanza kuusajili, ili kuwapa nafasi ya kushiriki katika tamasha la utamaduni mwaka huu.

Amesema idara imepata faraja baada ya mchezo wa ngware kufufuliwa, kwani michezo mingi ya utamaduni umekua ikipotea kwa sasa, hali inayopelekea kuwaunga mkono wale wanaoibua michezo hiyo kwa lengo la kuziendeleza tamaduni zao.

“Mchezo kama Nage, bao, karata, ngoma ya uringe, zuna, ngoma ya msewe wa wazee nao unakufa, saivi upo wa vijana ambao umeinuliwa ili ngoma hiyo iwepo,”alisema.

Anasema vijana wanahamu ya kushiriki sanaa lakini hawajuwi wapi sehemu ya kuanzia, hivyo ipo haja kwa wazee kuwarisisha vijana wao michezo hiyo ya utamaduni wa asili ya kisiwa cha Pemba.

VIONGOZI WA SERIKALI WANASEMAJE

Afisa mdhamini wa Wizara habari vijana Utamaduni na Michezo Pemba, Mfamau Lali Mfamau, amesema kuibuliwa kwa mchezo huo wa asili ni jambo la faraja, utaweza kuendeleza utamaduni wao wa asili ambao kwa kiasi kikubwa umeanza kupotea.

“Wizara umeupokea vizuri mchezo huo kama ilivyo michezo mengine, ni jambo la faraja kwa vijana kukubali ufufua mchezo wa ngware ambao wazazi wao walikua wakicheza,”amesema.

Aidha amewasihi vijana kuhamasishana kuenzi utamaduni wa kizanzibari, kuzingatia silka na desturi ya kizanzibar, kwa sasa vijana waliowengi umagharibi umewatawala.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Wete Dk.Hamad Omar bakari, kwa niaba ya mkuu wa Wilaya Micheweni, anaesema vijana wananafasi kubwa ya kuuendeleza mchezo wa ngware, kwani ni njia moja wapo itakayowasaidia kunua vipaji vyao na kuendeleza mila silkta na tamaduni za mIcheweni.

Amesema fursa zilizopo hatutoweza kuzifikia kama hatukurudisha mila silka za tamadunini zao za watu wa micheweni, kwani ngware kama ilivyokua michezo mengine.

MTAZAO WA VIJANA NI UPI KATIKA MCHEZO HUO

Yussuf Ali Khamis anasema, mtazamo wake ni kuona mchezo huo unatambulika ndani ya nchi kama ilivyo michezo mengine, na wao kupatiwa fursa ya kuutangaza kupitia maonyesho mbali mbali yanayofanyika nchini.

Nae Omar Khamis Kai anasema wanajitahi kushiriki katika matamasha mbali mbali, ili jamii iweze kuufahamu kama ilivyo michezo mengine ya asili katika Kisiwa Cha Pemba.

“Sisi tumeamua kujiripua moja kwa moja wapo watakaosema hatuna kazi za kufanya, lakini vizuri na sisi mchezo wa Ngware kujulikana na kuelekwa kama ni moja ya michezo ya asili Michweni,”amesema.

MAFANIKIO NA USHAURI KWA VIJANA

Ali Khamis Juma anasema kwa sasa bado hawajapata mafanikio makubwa, zaidi ya kuendelea kuutanga katika maeneo mbali mbali kwani ni mchezo mpya.

“Najua hautochukua muda kuzoeleka sasa unapofanyika, lazima watu wengi wajitokeze kuutama Ngware inachezwa vipi,”amesema.

Shamte Yunusi amewasihi vijana kuendeleza na kuukuza mchezo wa Ngware, kama ilivyo michezo mengine ikiwemo mpira wamiguu, basket boll, Ngoma ya Msewe lengo ni kutambulika kitaifa na kimataifa.

“Sisi hapa tunategemea kufika mbali baada ya kuusajili na kuutangaza, hii ni ajira kwetu vijana kama ilivyo ajira nyengine, utamduni wetu ndio urithi wetu kwa vizazi vya sasa na vijavyo,”amesema.

Wilaya ya micheweni mchezo wa Ngware umekua ni maarufu kama ilivyo aina ya andazi linaloitwa kombo alawi.

BAJETI WIZARA YA HABARI INESEMAJE JUU YA MICHEZO HUO

Kwa mujibu wabejeti ya Wizara hiyo 2023/2024 imesama Wizara kupitia idara ya utamaduni inaendelea kuhamaisha jamii kuhusu matumizi ya vifaa, mavazi, vyakyla na vitu vya kiasili kupitia vyombo vya habari, ambapo jumal ya kazi za sanaa 285 zimekaguliwa na kufanyiwa uhakiki kwa ajili ya kutolewa makosa ili ziweze kutumia hadharani.

Imesema jumla ya wasanii 15 na vikundi 43 vya sanaa na utamaduni vimesajiliwa upya kwa ajili ya kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na namba 7 ya baraza la sanaa.

MWISHO