Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar Mhe Valentina Andrew Katema amesema kuwepo kwa mashirikiano ya wadau mbali mbali katika kamati ya kusukuma mbele mashauri ya jinai kunasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza katika usikilizaji wa mashauri Mahkamani.
Ameyasema hayo katika kikao cha kamati ndogo ya kusukuma mbele mashauri ya jinai kilichofanyika katika ukumbi wa Mahkama Kuu Tunguu Zanzibar.
Aidha Mhe. Mrajis amesema uwepo wa vikao vya haki jinai inapelekea kupatikana kwa haki kwa wakati na viwango vinavyotegemewa.
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Daniel Shillah amesema vikao hivi vinalenga kugusa changamoto mbalimbali kuanzia mtuhumiwa anapokamatwa hadi anapofikishwa Mahkaman.
Kwa upande wake Daktari wa kitengo cha pf3 DR Salim Omar Mabrouka mesema vikao vinasaidia kubadilisha mawazo na uzoefu katika utendaji wa kazi zao.
Kikao hicho kimewashirikisha wadau kutoka jeshi la polisi. Vyuo vya Mafunzo. Hospital ya mnazi mmoja. Zaeka. Wakemia. Mamlaka ya madawa ya kulevya