NA ABDI SULEIMA, PEMBA.
KITIMTIMU cha mashindano ya Elimu bila Malipo ngazi ya Taifa kwa michezo mbali mbali yameendelea kutimua vumbi lake katika viwanja vinne tafauti ndani ya Wilaya ya Chake Chake.
Mchezo wa Mpira wa miguu uwanja wa chuo cha elimu ya amali Vitongoji asubuhi, skuli ya msingi Micheweni na jojo zikatoka bao 1-1, wakati wa saa nne Kitope ikaibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bungu.
Kwa upande wa uwanja wa Tenisi mchezo wa basket boll, sekondari wanawake skuli ya Uweleni imeibuka mshindi kwa vikapu 28-2 dhidi ya mitiulaya, skuli ya kwa mtipura ikaibuka mshindi kwa vikapu 27-17 dhidi ya kiboje, huku shamiani wakakubali kichapo cha vikapu 36-42 kutoka kwa mitiulaya.
Kwa upande wa skuli za msingi wanawake Mitiulaya imeshinda vikapu 18-2 dhidi ya Madungu na wanaume Urafiki imeibuka na vikapu 39-27 dhidi ya Chwaka.
Mpira wa mikono (hand boll) Sekondari wanawake Chanjamjawiri imeibuka na ushidi wa bao 9-3 dhidi ya Micheweni, skuli ya Michamvi ikakubali kipigo cha bao 12-3, wanaume Chanjamjawiri imeibuka na ushindi wa bao 13-4 dhidi ya Skuli ya Karume.
Kwa upande wa Msingi wanawake Chanjamjawiri imekubali kipigo cha bao 6-3 dhidi ya Karume, skuli ya Michamvi ikaibuka na ushindi wa bao 9-5 dhidi ya Kiswanduwi, kwa upande wa Msingi Skuloi ya Mjawiri nayo ikaibuka na ushindi wa bao 7-3 dhidi ya Karume.
Kwa upande wa sanaa za wimbo Sekondari, skuli ya Dunga imeibuka mshindi wa kwanza kwa kupata alama 356, ikifuatiwa na skuli ya Kinyasini Pemba na Mkwajuni zikipata alama 353, nafasi ya nne ikichukuliwa na skuli ya Ziwani Pemba ikiwa na alama 341.
Aidhga Ngonjera skuli ya Fujoni imeshika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 347, nafasi ya pili ikachukuliwa na skuli ya Mtoni Kidatu kupata alama 336, huku chasasa ikishika nafasi ya tatu kwa kupata alama 329, nafasi ya nne ikangukia kwa skuli ya Maendeleo iliopata alama 313.
Kwa upande wa maigizo vyuo vya amali, chuo cha Kwerekwe kimechukua nafasi ya kwanza kwa kupata alama 340 nafasi ya pili ikachukuliwa na Daya baada ya kupata 315, huku wasanii bora nafasi ya kwanza ikaenda kwa skuli ya Ziwani nafasi ya pili ikachukuliwa na skuli ya Mama Zaituni Fujoni.
MWISHO