Baadhi ya wazazi wamelalamikia kukosa huduma za vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao katika kituo cha utolewaji wa huduma hizo wilaya ya Chake chake kwa zaidi ya siku 5 kwa kile wanachojibiwa na watoa huduma kuwa ni kukosekana kwa huduma ya kimtandao katika ofisi ya wakala wa usajili wa matukio ya huduma za kijamii.
Hayo wameyabainisha wazazi hao kwa nyakato tofauti wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyefika eneo la tukio na kukumbana na wazazi hao.
Wamesema suala hilo limekuwa likisababisha hasara kwao kutokana na kutoka masafa ya mbali huku mchezo huo wa nenda rudi ukikosa kwa zaidi ya siku nne sasa ambao wanasema hofu yao ni kucheleweshewa na baadae kutozwa malipo katika huduma hiyo kwa kosa la kuchelewesha.
Aidha wanachoendelea kulalamikia baadhi ya wananchi hao wamesema ni kukosa taarifa maalum juu ya tatizo hilo ili kuweza kupumzika mpka yatakapokuwa sawa.
Wananchi hao ambao wengi wao ni akina mama wameiomba Serikali kuliangalia suala hilo ili kuwaondoshea usumbufu wanaoupata katika kuitafuta huduma hiyo muhimu.
” Nimeshakuja hapa mara ya nne hii kila nikija naambiwa mtandao unasumbua nisubiri nasubiri saa mbili mpka saa sita hakuna linalokuwa, sijui unasumbua nini wala mtandao gani unaosumbuwa nakosa kuelewa kibaya zaidi nashindwa kujua lini huduma hiyo itarejea ili itakaporejea ndio nije nisihangaike na mtoto kila siku” Alisema mama aliefika kufata huduma ya cheti cha kuzaliwa cha mtoto kutoka Mchanga mrima jina linahifadhiwa.
“Nauli ya nenda rudi kila siku juu ya suala hili hatunayo mimi nimekuja Jumatatu nikaambiwa nije jana sikuja leo nimeomba nauli nipo hapa ndio yale yale niliyoyakuta jumatatu natoka Vitongoji 800 nauli kila siku iko wapi .
” Changamoto zipo lakini wangeweka taarifa tukajua mana pale tukifika tunaandika namba za simu wangetutumia ujumbe tu kama huduma bado hazijarudi”. Alidai mama mwengine kutoka Vitongoji Chake chake.
“Tukiwauliza wanatuambia mfumo mfumo sisi tunajuaje kuhusu mfumo tunasumbuka bure na watoto kila siku kupoteza nauli zetu na tunakazi tele majumbani za kufanya tunaziwacha leo tunakaa apa tunasubiri ndege ituwe bandaraini “.
Miongoni mwa watoa huduma ambae sio msemaji wa taassisi hiyo kisheria jina lina hifadhiwa amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo amedai kuwa linasababishwa na mfumo wa Zan malipo pamoja na bank .
“Ili tuandike cheti nilazima kukamilika kwa stakabadhi za malipo na malipo mwananchi anapewa namba ya mfumo kwajili ya malipo na sisi tunasubiri uthibitisho ndipo tunatoa huduma hizo inapotokea zinachelewa kupitia huo mfumo wa kibenki na huduma huku zinachelewa ndio changamoto kubwa”.
Aidha amesema kuwa kuhusu usumbufu wanaoupata wananchi kwenda na kurudi bila kupata huduma hiyo ni kutokana na kushindwa kuwapa ahadi ya uhakika kwa vile changamoto hiyo ipo nje ya uwezo wao kuipatia ufumbuzi.
Alidai kuwa kutokana na taasisi hizo za malipo na wakala kuwa mbili tofauti hupelekea kushindwa kulidhibiti na kuwapa usumbufu wananchi wanaotaka huduma za vyeti vya kuzaliwa kwa watoto baadhi ya siku.
Harakati za kumtafuta Msemaji mwenye dhamana juu ya suala hili kisiwani Pemba zinaendelea kwa jili ya kupata ufafanuzi zaidi.