Tuesday, January 7

MAKALA: Udhalilishaji wa  mitandaoni  upo  tumia mitandao ya kijamii kwa ungalifu.

THUREYA GHALIB PEMBA.

Kuna ule msemao TAHADHARI KABLA ATHARI au mwengine husema mzaha mzaha hutumbua usaha,hii ni misemo ya Kiswahili inayokukumbusha kuchukua tahadhari ya kitu kabla hayajakufika  matatizo .

Udhalilishaji wa  mitandaoni  ipo  kwa kiasi kikubwa katika jamii na kwa watu wa matabaka mbalimbali huwa wanapitia.

Hakuna aliekuwa salama katika dunia hii ya kidigitali ili kuepuka udhalilishaji huu,ikiwa utakuepuka wewe basi mtoto wako ama ndugu yako lazima akutane nao ,na ni jambo linaloathiri akili sana.

Kwa kitalamu Udhalilishaji huu unaitwa (cyber bulling- saiba bulling),katika nchi nyingi udhalilishaji wa mtandao  haujawekea sheria bado ya kuwatia hatiani wafanyaji wa matendo haya.

Katika dunia ya sasa ambayo iko kiganjani kutokana na maendeleo ya mawasiliano. Mitandao haikimbiliki  imekuwa sehemu kubwa ya maisha yetu.

Kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania ya robo mwaka ya (1) ya mwaka 2022/2023 ambayo inahusu matumizi ya  huduma za simu.

Takwimu za ripoti hiyo  ya utendaji wa sekta ya Mawasiliano nchini zinabainisha mitandao mitano (5) ya kijamii inayotumiwa zaidi nchini Tanzania,    Hasa kulingana na kiwango kikubwa cha data iliyotumika kwa kipimo cha GB.

Aidha, ripoti hiyo imeeleza kuwa,  Mtandao wa kijamii wa FaceBook uliongoza kwa kurekodi (GB Bilioni 2.59), ukifuatiwa na YouTube wenye (GB Bilioni 1.91), kisha WhatsApp uliokuwa na (Bilioni 1.58), na TikTok ukiwa na (GB Milioni 999) ikifuatiwa na mitandao mingine.

Watumiaji wa interent wameongezeka kutoka 29,169,958 Juni 2022  hadim 31,122,163 september 2022 sawa na ongezeko na asilimia  6.7 %.

Hii ni ishara kuwa watumiaji wa simu janja na watumiaji wa mitandao ya kijamii ni wengi kutokana na matumizi hayo ya mtandao wa  mawasiliano ya kasi (Internet).

Hivyo uwezekano wa kutuma taarifa zenye kukiuka maadili na pia sharia ni mkubwa watu ambao hawana uwelewa na maadili ya matumizi ya mitandao.

Aidha,  tunavotumia mitandao kama vile facebook, whatsApp, instragram, tiktok nakadhalika, tunasahau kuwa tunavunja  sheria za kimitandao, hasa pale tunapotumia kwa kumkashifu mtu, kutuma picha zisizostahiki  kutumia taarifa za uwongo na mambo kama hayo huwa vinapelekea  kuvunja sharia hasa sharia ya Mtandao (Cyber Crime Act 2015).

Wengi wetu tunakuwa tunashangia  katika kurasa  tofauti tofauti na  mara nyengine tunatumia lugha chafu ,bila ya kuangalia na kujifikiria  maneno yale ungeambiwa wewe ungeweza kujisikiaje?.

Yule unaemnyanyasa kupitia mtandao anaweza kupata madhara mbalimbali ,anaweza kukosa kazi nzuri kwa saababu tu kunamtu alishapost picha zake za faragha  bila ridhaa yake huko nyuma na kupelekea kukosa kazi.

Tusichokijua ni kwamba yule unaemnyanyasa anaweza kujisikia mnyonge, kujidhuru na wengine mpaka kujiuwa. Hukosa raha pia anaweza kushindwa kufanya mambo ya maendeleo kutokana na udhalilishaji huo.

Kuna Visa vingi ambavyo watu mbalimbali wamemuhadithia mwandishi wa makala haya vinahusiana na udhalilishaji wa kimtandao.

WALIOKUMBANA NA KADHIA HIYO WANASEMAJE?

Nassour Muhammad ni mmoja wa waathirika wa udhalilishaji huo ,amefahamisha kuwa anarafiki yake wa kiume ambaye walikuwa wanaelewana sana na siku moja walienda kupunzika katika fukwe za bahari.

‘’Tulicheza mpira tulikula na  baadae tulipiga picha nyingi huku tukifurahia safari yetu hio ‘’Alielezea.

Aliendelea kuelezea  kuna siku moja walikuja kukosana na rafiki yake yule ,ndipo rafiki yake  aliamua kutuma  picha ambazo walipiga wakiwa fukwe za bahari.

‘’Kwa kweli picha alizotuma  sikufurahishwa nazo ,na kwa cheo nilichonacho ni ustadh wa madrasa  ,kitendo kile kilinifanya nijisikie vibaya na kuona aibu ata kumuangalia anaepita mbele yangu’’alielezea kwa masikitiko.

Alisema kwa haraka hatua niliyochukua nikumfuata yule rafiki yangu na kumuomba msamaha  na kutaka azifute picha zile ,aliofanya hivyo lakini watu wakiwa wameshaziona.

Muathirika mwengine wa udhalilishaji huo ni Amriya Khalid alilezea kuwa anapitia udhalilishaji huo siku baaada ya siku, yote hayo yanamfika kwa sababu ya maumbile yake ni mnene.

Alisema akituma picha yake yoyote katika mitandao ya kijamii  watu ‘’UTAPASUKA’’ ‘’PUNGUZA KULA WEWE’’PUNGUZA KILO WEWE’’ na maneno mengine ya kukosesha raha.

Akizungumza huku sauti yake ikiwa inatetemeka alianza kutoka machozi na kutiririka katika wajihi wake na kunambia kuwa ni maumivu makubwa anayoyapata  akitumiwa  jumbe  kama hio.

‘’Kuna muda nakaaa nawaza huku nikilia peke yangu ,Siupendi mwili nilionao na najitahidi kufanya kila njia niweze kupungua pengine hilo litaweza kunisaidia kuepukana na unyanyasaji huo’’alisema Amriya.

Kuna siku niliamka asubuhi na mapema nikajitarisha kuelekea kiwanjani kufanya mazoezi mimi na majirani zangu ,wakati tupo katika mazoezi mmoja wa jirani yangu alichukua video na kupost katika whatsapp yake.

Badae nilimuona anacheka huku akiwaonesha wengine ujumbe uliotumwa katika simu yake  ujumbe huo ulikua unasomeka hivi  nanukuu.

‘’huyo tembo nae anafanya mazoezi ili apate nguvu kwa kula chapatti saba au’’ Kwa kweli sikuweza kuvumilia nililia sana alisema Amriya kwa uchungu mkubwa.

Alisema hakuna kitu kibaya kama mtu akawa ana kitu kinamla ndani kwa ndani ,ambacho kinaumiza kimwili na kiakili na huku ukiwa huna mtu wa kumueleza matatizo yako,ndipo unapomkuta mtu amejinyonga au kujidhuru.

Hivyo Udhalilishaji wa mtandao ni mbaya sana usichukuliwe kirahisi,unathiri akili ,unakukosesha kujiamini mbele za watu vilevile unakupa uduwazi.

Tukiachana na Amriya kuna muathirika mwengine wa udhalilishaji huo ambae hatutaka jina lake litajwe,alieleza kuwa udhalilishaji huo ulimpata na aliyefanya kitendo hicho alikuwa ni mpenzi wake.

Alisema alikua mjinga sana kumuamini mwanamme yule na kufanya kila kitu anachotumwa  na mwanamme huyo,hadi siku moja alipomuomba kumtumia picha yenye kuonesha sehemu zake za siri .

Alisema alitakaa kutuma picha hiyo  , ndipo mpenzi wake huyo  alipomuliza unaninyima kitu ninachokipenda kwa hiyo huniamini,kama ndio hivo tuachane na usinitafute.

‘’Kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa mwanamme yule nilingia chooni na kupiga picha na kumtumia huku nikionekana sehemu tofauti tofauti za mwili wangu’’Alifafanua.

Baada ya hapo alifurahi sana na nikaweza kuliokoa penzi langu ,sasa ndio ikawa ndio tabia yake kuniomba nimtume picha hizo kwa kuhofia kumkosa yeye nikawa natuma  huku yeye akinishukuru na kunisifia.

Hadi siku ambayo mmoja wa Rafiki wa mpenzi wangu aliponiita na kuomba kuongea na mimi,alinifahamisha kuwa  picha zangu za utupu ninazomtumia mpenzi wangu anawaonesha marafiki zake wanapokuwa katika maskani hiyo.

Nilisisimkwa mwili huku nikiwa sijui lakufanya ,nikachukua hatua za kumfata yule mwanamme na kumuliza taarifa nizizozipata zina ukweli wowote?,cha kushangaza  alinijibu majibu mabaya sana na kusema niachane nae .

Kitendo kile kiliathiri sana ,nilidhofika mwili ,jamii ikanichukulia kama ni mtu muhuni nisiejiheshimu ,nilitolea mifano mibaya katika familia za watu nilikosa mpaka mume wa kunioa kwani anapokuja anapewa taarifa ya picha zile.

Pamoja na hayo naiomba jamii hasa wanawake wasiwaamini wanaume sana mpaka kufikia hatua ya kujidhalilisha kwa kutuma picha zako za utupu ili kunusuru penzi lake.

Katika Mahojiano na shirika na Utangazaji la Uingereza la BBC  takriban miezi 6 nyuma Waziri wa habari mawasiliano na teknolojia yan habari  nchini Tanzania  Nape Nnauye  amesema tatizo la picha ngono kutumwa katika mitandao ya kijamii ,sio salama kwa maadili ya kitanzania na serikali itatumia mifumo yake ili kulinda watoto ambao ndio waathirika wakuu.

Alisema  tatizo hili ni kubwa si Tanzania pekee bali ni nchi nyingi duniani. Hivyo,  Serikali inawajibu wa kuwalinda watoto na  inaonya vikali udhalilishaji mtandaoni .

Alisema kuna udhalilishaji mkubwa kupitia mitandao ya kijamii ,wajibu wa serikali ni kutoa fursa za mawasiliano  kwa  ajili ya maendeleo na sio kutumika mawasiliano hayo kuumiza wengine na kufanya vitendo vya kihalifu. Hivyo serikali itahakikisha inaendelea kulinda uhuru wa mtu mwengine usingiliwe  hasa faragha.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ni tasisi ya serikali yenye jukumu la kusimamia sekta ya mawasiliano Tanzania imeanzishwa  kwa mujibu wa sheria no12 ya mwaka 2003.

 

 

Mwanasheria kutoka  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA) Zainab Khamis alisema Unyanyasaji wa kijinsia kupitia mitandao bado haijaripotiwa vya kutosha na kuchukuliwa kama ni jambo la kawaida wakati unaathari kubwa kwa anaetendewa .

Alisema mwanasheria huyo hata katika Mahakama  hakujakuwa na miundombinu imara ya kusikiliza kesi hizo hasa kwa kutumia  ushahidi wa video au picha.

“Sheria ya makosa ya mtandao iliyopitishwa na bunge tarehe 1 Aprili 2015 na kuaidhinishwa na Rais wa  Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  MheshimiwaJakaya Mrisho Kikwete April 25 mwaka 2015.

Kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha kanuni ya adhabu (The penal code)Sura ya 16 ya sheria ya Tanzania inafahamisha kuwa kutokujua sheria haku muondolei hatia mtuhumiwa.

Jamii inatakiwa kuelewa kwamba kutuma picha ya mtu bila ridhaa ,kumkutana mtu mitandaoni ,kutapeli watu kupitia mitandao au kufanya jambo lolote linakalopelekea athari kwa mwengine ni makosa kisheria.

Serikali tunaiomba iweze kuweka mikakati maalum ya kupambana na kesi hizi,wanaothirika wengi ni wanawake kuliko wanaume.

 

Vilevile Mitandao inafaida nyingi kama vile, kupata habari, kujifunza, kufanya biashara, ikiwa tutaitumia vizuri ,ni vyema basi tukaitumia vizuri ili iweze kuleta  tija kwa Jamii na Taifa kwa ujumla .