Thursday, January 16

WALIMU wapewa neno  ya Siku ya walimu duniani  SUZA Mchangamdogo, Pemba.

Katibu Mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya amali zanzibar Dkt, khamis Abdalla Said akizungumza na walimu kwa niaba ya waziri wa elimu na mafunzo ya amali zanzibar Lela Mohammed Mussa wakati wa ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya walimu duniani huko katika ukumbi wa chuo cha uwalimu mchangamdogo Pemba
Ofisa Mdhamini wa Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Kisiwani Pemba Mohammed Nassor Salim akizungumza na walimu katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya walimu duniani katika ukumbi wa chuo cha uwalimu Mchangamdogo Pemba,
Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar (ZATU) Haji Juma Omar akisoma taarifa ya chama hicho katika ufunguzi wa kongamano la maaddhimisho ya siku ya walimu duniani katika ukumbi wa chuo cha uwalimu Mchangamdogo Pemba,
Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt, Mohammed Said Mohammed (Dimwa) akizungumza na walimu katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya walimu duniani katika ukumbi wa chuo cha uwalimu Mchangamdogo Pemba.

NA SAID ABRAHMAN-PEMBA.

WALIMU wametakiwa kujiunga na Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU) ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutatua changamoto zao.

Hii itaweza kuwasaidia walimu hao  kupaza sauti zao Kwa pamoja katika kutetea haki zao .
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Kwa niaba ya waziri wa elimu na Mafunzo ya amali Lela Mohammed Mussa wakati wa ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya walimu duniani yaliyofanyika huko katika Ukumbi wa Chuo Cha SUZA Mchangamdogo, Pemba.
Dkt, Khamis alieleza kuwa Wizara ya elimu imekuwa ikishirikiana na Chama Cha Walimu ZATU ili kuona zile changamoto ambazo zinawakabili walimu zinatatuliwa Kwa haraka.
“Wizara imekuwa karibu sana na Chama Cha Walimu katika kushirikiana pamoja kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya elimu Kwa lengo la kurahisisha azma ya Serikali ya awamu ya nane (8) Kwa kuimarisha mazingira ya ufundishaji katika skuli zote ili kuongeza ufaulu Kwa wanafunzi,” alifahamisha Dkt, Khamis.
“Niwaombe walimu wote wajiunge na Chama Cha Walimu Zanzibar ZATU ili kuwa na nguvu ya pamoja ili waweze kusikilizwa na kushirikishwa kwani ni vigumu kumsikiliza mwalimu mmoja mmoja katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbali mbali,” alieleza  Dkt, Khamis
Sambamba na hayo Katibu huyo alifahamisha kuwa Kwa Sasa Wizara imeanza mchakato wa kuyafanyia kazi malalamiko ya walimu ambayo waliyatoa mbele ya Rais katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho ikiwemo posho la usafiri.
Mapema Dkt, Khamis aliwataka walimu hao kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Serikali Kwa kuwajika katika kazi zao na kuepukana na tabia za uvivu au utoro kazini ambazo zitaweza kuwaharibia sifa zao.
“Niwaombe wale ambao hawaendi sambamba na Serikali ya awamu ya nane (8) wabadilike Kwa kufanya kazi Kwa bidii zaidi Kwa maslahi ya taifa lao,” alisema Katibu huyo.
“Katika kipindi hichi tumepata mafanikio mengi katika sekta ya elimu kwani Muheshimiwa Dkt, Hussein Ali Hassan Mwinyi amepania katika kuimarisha huduma za kijamii na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo Bora,” alieleza Dkt Khamis.
Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mohammeda Said Mohammed (Dimwa) ametoa Siku 30 Kwa Serikali ili kuhakikisha imeunda tume ya utumishi ya walimu Zanzibar .
Alisema kuwa endapo tume hiyo itaundwa itaweza kuondoa malalamiko Kwa walimu hao pamoja na kuweza kuwasaidia kutatua changamoto zao zinazowakabili.
“Nitoa Siku 30 Kwa Serikali kuhakikisha tume ya utumishi ya walimu Zanzibar inaundwa na Mimi nachukua ahadi ya kukutana na Rais wa Zanzibar Dkt, Hussein Ali Hassan Mwinyi ambae ni Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kuona jambo hili linafanikiwa,” alisema Dimwa.
Dimwa aliwahakikishia walimu hao kuwa suala la tume ya utumishi ya walimu halina mjadala wowote na kuahidi kuonana uso Kwa uso na Rais wa Zanzibar Dkt, Hussein Ali Hassan Mwinyi ili kuona tume hiyo inaundwa Kwa haraka sana.
Aidha Naibu huyo  aliwataka walimu hao kutekeleza wajibu wao na kutimiza malengo waliyopangiwa ili kuleta ufanisi mzuri wa kazi yao.
Sambamba na hayo Dimwa alimtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar kukaa pamoja na waziri wa uchukuzi wa Muungano wa Tanzania Profesa Makamw Mbarawa mnyaa kuona ndege za shirika la ndege Tanzania zinafanya shughuli zake ndani ya Kisiwa Cha Pemba.
Alisema kuwa ameshangazwa sana kuona Ofisi za shirika Hilo Pemba ipo lakini hakuna hata safari yeyote ambayo inafanywa na ndege za shirika Hilo.
Nae Ofisa Mdhamini wa Wizara ya elimu na Mafunzo ya amali Kisiwani Pemba Mohammed Nassor Salim alikipongeza Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU) Kwa kusaidia sana kuleta utulivu Kwa walimu, kwani walimu wanapokuwa na malalamiko pamoja na hoja zao wanajua sehemu ya kukimbilia.
Aidha Ofisi huyo alieleza kuwa mbali na kazi hiyo lakini pia Chama kimekuwa kikisaidia mambo mbali mbali mbali katika kunyanyua sekta ya elimu nchini.
“Tunampongeza sana Dkt, Hussein Ali Hassan Mwinyi Rais wa Zanzibar Kwa juhudi zake kubwa anazozichukuwa katika kuimarisha sekta ya elimu nchini,” alisema Ofisa huyo.
Mapema akisoma risala ya Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU) Katibu Mkuu wa Chama hicho Haji Juma Omar alieleza kuwa kazi kubwa ya Chama hicho ni kuwaunganisha walimu wote wa Zanzibar, sambamba na kuwahimiza walimu kutekeleza wajibu wao.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuwepo Kwa tume ya utumishi ya walimu Zanzibar kutatua changamoto zinazowakabili walimu Zanzibar”.
                  MWISHO.