NA ABDI SULEIMAN.
MKURUGENZI wa Biashara wa bank ya watu ya Zanzibar Eddie Mhina, amesema PBZ inathamini sana wateja wake, ndio maana wakawa wanafanya vitu tafauti tafauti katika kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kukirudisha kwa wananchi kile wanachokipata.
Alisema katika kutilia mkazo malengo yao ya kutoa huduma bora, imefungua kituo cha huduma kwa wateja kwa kutumia simu na mteja anaweza kupiga simu namba 0800000004, na kutatuliwa changamoto zake, pamoja na kuongeza vituo vipya, mawakala kila maeneo na ATM.
Mkurugenzi huyo aliyaekeza hayo, katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja wa bank hiyo, hafla iliyofanyika mjini Chake chake Mkoa wa kusini Pemba.
“Sisi kama benk wiki hii tutaiadhimisha mwezi mzima huu, katika kutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuwapatia kilichobora na kuridhika na huduma tunazozitoa kwa wateja wetu,”alisema.
Aidha mkurugenzi huyo aliwashukuru wateja wao, kwa uwaminifu wanaoutoa kwa bank hiyo katika kuweka fedha zao na kufanya miamala mbali mbali ya kifedha ndani na nje ya nchi.
Nae Mkurugenzi Rasilimali watu na utawala PBZ Zanzibar Abdul Bilali Kandori, aliwataka wananchi na wafanyabiashara kuendelea kuitumia bank kwa kuweka amana zao, pamoja na kuzitumia fursa mbali mbali za mikopo zinazotolewa.
“PBZ ni miongoni mwa bank kongwe nchini na imekua ikitoa huduma mbali mbali mbali kwa wateja wao, vizuri wafanyabiashara kuendelea kuitumia bank hii kwa kuweka amana zao pamoja na kutumia fursa za mikopo inayotolea hapo,”alisema.
Kwa upande wake meneja wa masoko PBZ Zanzibar Seif Suleiman Mohamed, alisema kwa sasa PBZ ina ATM 45 Tanzania mzima na wametoa Visa kadi kwa wateja wao, ili waweze kupata fedha sehemu yoyote ile duniani, huku wakia na mawakala zaidi ya 1000 Tanzania na wakiendeka kutoa huduma hiyo.
Nao wateja wanaopata huduma katika bank hiyo, wautaka uongozi kuongeza watoa huduma za fedha madirishani, hususna mwisho wa mwezi ili kupunguza msongomano wa wateja wao kipindi hicho kinapofika.
Khamis Mohamed mkaazi wa ngwachani, alisema wamekua wakipata mashirikiano mazuri na wafanyakizi wa bank hiyo, pale wanaotaka kuweka kutoka na kuomba mikopo.
Hata hivyo aliuomba uongozi kuhakikisha wanatumia mwezi huu wa huduma kwa wateja, kwa kufika vijijini kwenda kutoa huduma za kibenk pamoja na kusaijili wateja wapya.
MWISHO