NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Tigo Zantel Zanzibar Azizi Said Ali, amewataka watoa huduma wa kampuni hiyo kuzidisha juhudi katika utoaji wa huduma zao, ili kufunga mwaka kwa matokeo mazuri.
Alisema iwapo watoa huduma hao wataendelea kutoa huduma bora basi mwaka utakua mzuri kwao na ushindi unaweza kurudi tena katika kisiwa cha Pemba.
Mkurugenzi huyo aliyaeleza hayo wakati wa usinduzi ya Wiki ya Huduma kwa wateja, iliyofanyika katika stendi ya magari Konde, pamoja na kwenye tafrija ya chakula cha usiku huko Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi Mkuu, Meneja wa Tigo Zantel Kanda ya Pemba Farouk Ahmed, aliwapongeza wafanyakazi na watoa huduma kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma bora kwa wateja wao, hali itakayopeleka Pemba kushika nafasi ya kwanza kwa zoni ya Zanzibar.
“Sina budi niwashuhuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa munayoendelea kuifanya, endeleni kutoa huduma vizuri kwa jamii ili sifa yenu ya Pemba iendelee kubakia” alisema Forouk.
Nae Meneja mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Zanzibar, kutoka kampuni ya simu za mkononi Tigo Zantel Fatma Mohd Khalfan, aliwataka watumiaji wa mitandao huo wanapopata matatizo katika utumiaji wao, wasisite kutoa taarifa ili yaweze kutatuliwa.
Alisema wameamua kufika konde kwa sasabu ya kusikiliza malalamiko ya wateja wao katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya mawasiliano.
“Malalmiko yamekua mengi ya wateja yanatoka huku Konde, ndio maana tumekuwepo hapa toka asubuhi lengo ni kusikiliza malalamiko hayo ili kwenda kuyapatia ufumbuzi,”alisema.
Akitaja changamoto kubwa inayojitokeza kwa wateja wao mji wa Konde, alisema ni kushuka kwa network kitu ambacho watakwenda kukifanyia kazi ili wananchi wote wapate mawasiliano mazuri kama ilivyo maeneo mengine.
Alisema kwa sasa wameshaanza Unguja kurekebisha kila sehemu ambayo huduma inasusua, baada ya kumaliza hapa safari itakayofuata ni kufika Pemba.
“Sisi kazi yetu ni kutoa huduma bora kwa wananchi, lakini watumiaji ndio wanajua zaidi kuhusu huduma zetu, hivyo tutayachukua malalamiko yao na tutakwenda kuyashuhulikia na yataisha,”alisema.
Akizunguzmia suala la utapeli wa mtandaoni unaoendelea hivi sasa, aliwashauri watumiaji wa Tigo Zantel kutokufanya biashara za mtandao kama mtu humjuwi, na hakikisha biashara wanayofanya inafika ndio waweze kufanya miamala ya malipo.
Nae Mnufaika wa huduma ya Tigo Zantel, kutoka Konde Omar Khamis Kombo, alisema Tigo Zantel imekua na mafanikio makubwa kwao, kwani imawasaidia kwa kiasi kikubwa katika utumaji na upokeaji wa fedha na kuachana na mtindo wa kuchukua fedha mkononi au keshi.
Akizunguzmia changamoto, aliuomba mtandao huo kuwadhibiti matapeli wanaotapeli wateja wao, kwani wamekua wakiwarudisha nyuma kimaendeloe.
MWISHO