Monday, November 25

Wanafunzi washauriwa kusoma ubaharia

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

WANAFUNZI wa skuli ya Sekondari Dr Amani Micheweni, wameshauriwa kuzitumia fursa zinazopatikana katika bahari, kwani nchi inahitaji mabaharia wengine ambao watakaoweza kuendesha meli za ndani na za kimataifa.

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa kitengo cha habari ZMA Zanzibar Makame Ussi, wakati alipokua akizungumza na wanafunzi, na wavuvi katika bandari ya Tumbe kwenye wiki ya bahari hivi karibuni Kisiwani Pemba.

Alisema bahari ni sehemu inayohitaji wataalamu wengi zaidi na imeajiri watu wengi, kuliko sekta yoyote ile duniani hivyo bado fursa zipo katika bahari.

Alisema hivi sasa sekta ya bahari nayo itakua inaheshimika kama ilivyo sekta nyengine, kwani imekua na mchango mkubwa duniani kote, kwenye suala la usafirishaji wa mizigo.

Naye mkuu wa Kitengo cha habari shirika la bandari Zanzibar Hassan Juma Abuu, aliwataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo kwani sekta ya bahari ni muhimu ni sekta kubwa.

Aliwasihi wanafunzi baada ya kumaliza masomo kujiunga na chuo cha bahari, kwa ajili ya kujifunza mambo mengi yanayohusiana na bahari ikiwemo suala la usalama wa bahari.

Naye mwakilishi kutoka shirika la meli Zanzibar Salum Abdalla, alisema wakati umefika mabahari wa meli kuhitajika, hivyo wanafunzi wanapaswa kuzitumia fursa za kusoma fani ya ubaharia, kwani mategemeo ya serikali bandari ya shumba itakapokamilika wananchi wa micheweni wataweza kufanya kazi.

Kwa upande wake Mkufunzi Msaidizi DMI Jesca Madete, aliwataka wanafunzi kuhakikisha wanajiunga na chuo cha bahari kwa lengo la kupata elimu mbali mbali ikiwemo ubaharia.

“Wakati umefika wa kutunza rasilimali za bahari kwa vizazi vivavyokuja, wazee wanapitia mengi ili kuhakikisha bahari wanatunza mazingira yote ya bahari na bahari kuendelea kubaki salama,”alisema.

Nae Afisa Mawasiliano na Uokozi kutoka KMKM Pemba Malik Makame Hussein, alisema kesi 250 za watoto kufa baharini zimetokea mwaka huu, tayari wamejipanga kupunguza matukio hayo baada ya kuanzisha kituo cha kutoa mafunzo ya kuongelea na uzamiaji ili kuwasaidia watoto.

“Serikali imeweka vituo vya uokozi vitatu, lengo pale linapotokea tatizo iwe rahisi kwenda kutoa uokizi, ikizingatiwa hili sua la uokozi sio la serikali bali kila mtu linamuhusu,”alisema.

Mwalimu Mkuu skuli ys Dk Amani Sekondari Micheweni Jabu Haji Abrahman, alisema wataka wanafunzi kutambua kuwa serikali imewekeza mkakati katika suala la uchumi wa buluu, ili kuifikia huko lazima wanafunzi wajiunge na chuo cha bahari kupata elimu sahihi ya matumizi ya bahari.

Naye Iddi Mwalimu Iddi mvuvi katika bandari ya Tumbe, aliwataka watu wa bahari kupiga vita suala la uvuvi haramu kwani unachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mazingira ya bahari.

Nao wanafunzi wa skuli ya Dk.Amani wamewashuhuru wataamalu wa bahari, kwa kuwafumbua macho kwani awali waliiyona sekta ya bahari ni sehemu ambayo mtu ameshindwa kimaisha.

MWISHO