Thursday, January 30

Washiriki wa jukwaa la jamii watakiwa kuchukua hatua

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.

AFISA mdhamini Wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali, amesema Jukwaa la Jamii, usawa wa kijinsia na masuala ya udhalilishaji ni jukwaa moja muhimu kwa maslahi ya tifa, kwani kuna mambo mengi yanayohusiana na udhalilidhaji yanatakiwa kuwa mtambuka kwa sasa.

Alisema kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuchukua hatua, ili kuona matukio ya udhalilishaji yanatokomezwa, pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika kuhakikisha kesi hizo zinatolewa hukumu mapema.

Kauli hiyo aliitoa wakati akifungua jukwaa la jamii, usawa kijinsia na masuala ya udhalilishaji lililoandaliwa na Idara ya katiba na msaada wa kisheria kwa ufadhili wa shirika la UNDP na kufanyika mjini Chake Chake.

“Rais Dk.Mwinyi ameanzisha mahakama maalumu ya kuhshuhulikia kei za watoto, lazima na sisi tuunge mkono kwa kuyafikisha matukio hayo katika vyombo vya sheria,”alisema.

Aidha alisema mahakimu wamejipanga katika kesi hizo hazichelewi, zinakwenda kwa kasi kubwa kwani wanatekeleza maagizo ya serikali.

Akizungumzia watoa msaada wakisheria, Mdhamini huyo amewataka watoa msaada wa kisheria kwenye maeneo jamii, kutambua kuwa wananafasi kubwa kuona wanatoa msaada wakisheria bila ya kufanya usuluhishi wa kesi hizo.

“tunapaswa kuhakikisha tunapotoa elimu ya msaada wakisheria, tunatakiwa kujiweka mbali mbali na masuala la usuluhishi wa kesi, badala yake tunakua mstari wambele kuhakikisha kesi zinafika kwenye vyombo vya kisherai.

Aidha alisema wizara afya jukumu lao kubwa ni kuona wanakamilisha ushahidi wa kitaalamu, kwenye matukio ya udhalilishaji, huku akiwataka kila mhusika kwenye kesi hizo kitumiza majukumu yake kwa wakati.

Akizungumzia suala la takwimu, alisema ipo haja kwa taasisi zote kutumia takwimu kutoka ofisi ya mtakwimu mkuu na sio kila taasisi kua na takwimu zake.

Mapema Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais katiba, sheria utumishi wa uuma na utawala bora Pemba Halima Khamis Ali, amelishukuru shirika la UNDP, kwa msaada wao wanaoendelea kutoka katika kuhakikisha upatikanaji wa haki unafanikiwa.

Aliwataka wahusika wa jukwaa kulitendea haki, kwa kuhakikisha mabadiliko makubwa yatapatikana, kwa kulitendelea haki na kuleta matokeo chanya.

Nate Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wakisheria Zanzibar Hanifa Ramadhani Said, alisema Rais wa Zanzibar amekua mstari wambele kupiga vita masuala ya udhalilishaji, hali iliopelekea kuanzishwa kwa mahakama maalumu ya watoto, ambapo jitihada mbali mbali amekua akizichukua.

Alisema jukwa hilo litaondokana na maazimio ambayo yatawasaidia kupambamba na kuondokana na matukio ya udhalilishaji, vipi wataweza kuwasaidia wahanga, wazazi na jamii vipi inakua nao na kuachana kuwapatia majina mabaya.

MWISHO