NA MGENI KHAMIS, PEMBA
TIMU ya Hard Rock inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar, imekabidhiwa vifaa mbali mbali vya michezo na Bank ya NMB Pemba, ili iweze kufanya vyema katika ligi hiyo.
Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo imefanyika katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo Ngerengere Jeshini, huku viongozi mbali mbali wa timu na wachezaji wakishuhudia.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa bank ya NMB Tawi la chake chake Pemba Hamad mussa Msafiri, amesema NMB inafahamu uwepo wa timu huku akiitaka timu ya Hard Rock kuzidisha juhudi katika michezo yao ili iweze kuepukana na kushuka daraja.
Alisema NMB inatabua timu hiyo kama imepanda daraja, ndio maana imeamua kuwatia nguvu na kuwapa hamasa kutokana na kutambua mchango unaotolewa na timu hiyo.
Aidha aliwahidi wachezaji iwapo wakifanya vizuri katika ligi hiyo, wataendelea kunufaika na misaada mbali mbali ya vifaa vya michezo kutoka NMB.
“Kwa sasa nawaombeni mupokeee hichi hichi kidogo tulichojaaliwa kupata na kuwaja kuwakabidhi najua kitawatia nguvu na kufanya vizurio katika mashindano yenu,”alisema.
Kwa upande wake lutein kanali Julius Emmanuel Nkwabi, ameishukuru bank ya NMB kwa msaada walioutoa na ameahidi kuwa timu yao itafanya vyema kadiri ya uwezo wao na kufikia malengo mazuri.
Nae kocha wa Timu ya Hadrock Ussi Ali, ameishukuru bank ya NMB kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani vitawasaidia na kuwapa nguvu katika mapambano na kuiendeleza tiomu mbele.
Aidha vifaa vilivyokabidhia, Jezi, bukta, stokini na mipira.
MWISHO