Thursday, January 16

ZSTC yatakiwa kuharakisha upelekeaji wa fedha.

 

NA ABDI SULEIMAN,PEMBA

WAKULIMA wa karafuu Kisiwani Pemba ambao wanapokelea fedha zao kupitia TigoPesa, wameliomba shirika la ZSTC kuharakisha upelekaji wa fedha mapema kwenye kampuni ya Tigo Zantel, ili waweze kupata fedha zao mapema na kuepuka wakulima kuchukua fedha zao mkononi.

Alisema iwapo fedha hizo zitachelewa kufika kwenye kampuni hiyo na wao kuchelewa kupatiwa, itapelekea wakulima kukata vibali vingi na kuchukua fedha mkononi wakati mitandao sasa imerahisisha kila kitu.

Wakizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi zawadi huko ZSTC Chake Chake, kwa wakulima waliochangua huduma ya tigoPesa kupokea malipo yao ya karafuu kwa awamu ya pili.

Mkulima Mohamed Said Salum kutoka Mkoani, alisema huduma ya kupokea fedha kwenye mtandao wa simu ni nzuri kwao, kwani fedha zake zinakua salama muda wote na anaweza kutoa sehemu yoyote pale anapozihitaji.

“Kitu cha msingi ZSTC kufikisha fedha mapema na wakifanya hivyo basin a sisi tutapatiwa fedha zetu kwa wakati, leo unauza gunia zako 10 na wasiwasi huna baada ya muda saa moja tu fedha zako zinaingia na unaweza kufanya shuhuli nyengine,”alisema.

Aidha Mkulima huyo aliwataka ZSTC kuboresha huduma zao, ili wananchi wengi wavutike kupokelea fedha kwenye mitandao na sio kuchukua fedha mkononi hali inayoweza kusababisha matatizo baadae.

Nae Mkulima Mohd Khamis Ali kutoka Tibirinzi, aliishukuru kampuni ya Tigo Zantel kwa kuamua kutoa hamasa kwa wakulima wa karafuu kila mwezi kuwapatia zawadi, kwani kufanya hivyo kutaongeza hamasa zaid kupokelea fedha zao kupitia tigoPesa.

Hata hivyo aliwataka kuboresha zaidi mitandao huo, kwani fedha zinaweza kuwekwa mapema lakini kufika kwa mteja zikachelewa kutokana na mtandao wenyewe.

Mapema Meneja wa TigoPesa Zanzibar Salum Nassor Mohamed, aliwashukuru wateja hao kwa uamuzi wao wa kutumia tigopesa kupokelea fedha zao, kwani ni njia salama kwa fedha zao hata simu ikipoteza fedha haziwezi kupotea.

Aidha aliwataka wakulima kutumia huduma ya tigoPesa, ili kuisadia serekali kuokoa gharama ya matumizi makubwa ya fedha pale zinapopotea na kuisadia jamii kwa kutoa ajira za mawakala kupitia fedha za makato yao.

Alisema Tigo Zantel ilianza kupokea malipo ya karafuu msimu wa  mwaka 2021-2022, ambapo takribani bilioni 40 walilipwa wakulima, msimu wa 2022-2023 wakulima walipokea Zaidi ya billioni 14 na msimu wa 2023-2024 bado wanaendelea.

“Hii inaonesha wazi kuwa TigoPesa ni mfumo ambao uko salama, ndio maana tumeweza kupokea wakulima zaidi ya elfu kumi (10,000) wameshalipwa fedha kupitia TigoPesa kupitia mauzo yao ya karafuu,”alisema.

Hata hivyo aliwashauri wakulima kutumia huduma hiyo katika kupokea fedha zao, ni njia salama na rahisi kutumia na unaweza kutoa fedha popote ulipo kwani wanamakala Zaidi ya elfu nne wapo.

Aidha aliwataka wakulima wa karafuu ambao bado hawatumii huduma ya tigopesa, watumie kwani ni awamu ya pili kutoa zawadi na bado zawadi zipo na wanaendelea kutoa hadi pale msimu wa karafuu utakapomalizika.

Kwa upande wake mdhamini wa shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Pemba Abdalla Ali Ussi, amewashauri wakulima wa karafuu kukubali kuendelea kupokea malipo yao kupita kampuni ya simu ya mkononi kwani ni rahisi na salama.

Alisema zaidi ya asilimia 84 ya wateja, bado wanapokea fedha zao mkononi, asilia 13 wanatumia huduma ya tigo pesa na kupeleklea kuwa njia ya pili inayopendwa na wateja.

 

Alisema shirika la ZSTC inatumia njia tatu za kulipa fedha kwa wakulima, baada ya kuuza karafuu zao katika shirika hilo, moja Bank, TigoPesa na pesa mkononi kwa wale wakulima wadodo wadogo.

Aidha alisema kuna baadhi ya wakulima bado wanapokelea fedha mkononi, hata kama wanakarafuu nyingi kwa kuataka vyeti tofauti jambao ambalo sio nzuri kwa usalama wa fedha zao.

Hata hivyo aliipongeza kampuni ya Tigo Zantel, kwa ahadi yao walioitoa ya kuwapa hamasa wakulima wa zao la kafaruu kwa kuwapatia zawadi kwa awamu ya pili, wakulima wanaofanya vizuri kwenye uzaji wa karafuu kwa kutumia huduma ya tigopesa.

 

MWISHO.